Kufuru! Simba Watua Kibabe Dar

Kikosi cha Timu ya Simba wenye masknani yake katika Mtaa wa Msimbazi kimewasili Jijini Dar es Salaam leo mchana, Ijumaa, Januari 14, 2022 kikitokea visiwani Zanzibar walipokwenda kushiriki Michuano ya Mapinduzi Cup.

Simba wametua baada ya kubeba ubingwa wa kombe hilo kwa kuichapa Azam FC, jana usiku katika mchezo wa Fainali kwa ushindi wa goli 1-0, uliopigwa katika Dimba la Amaan, ambapo bao pekee la Simba lilifungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati.

Hiki ni Kikombe cha Kwanza kwa mwalimu wa Kikosi hicho, Pablo Franco Martin ambae amejiunga na Wekundu hao miezi michache iliyopita.

Hii ni rekodi kwa Simba kuingia fainali na kuchukua kombe hilo kwani kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa akifika hatua ya fainali lakini anapigwa. Huu ni Ubingwa wa nne wa Simba kwa Kombe la Mapinduzi.


Toa comment