The House of Favourite Newspapers

Kuhamia Nyumba Mpya… Mobeto Yamkuta

0

DAR ES SALAAM: Baada ya picha za mjengo wake mpya uliopo maeneo ya Mbezi Beach, Dar kuvuja, mrembo Hamisa Mobeto yamemfika baada ya wananzengo kubumburua yaliyokuwa yamelala, Amani lina ubuyu wote.

 

Mapema wiki hii, picha za mjengo huo wa ghorofa zilivuja kupitia kurasa za wapambe wa Mobeto katika mtandao wa Instagram na ndipo watu walipoibuka na maneno ya ‘kumchapa’ mrembo huyo.

 

“Hawa wasanii jamani wana mambo ya hovyo sana, wanapenda sana hizi show off halafu baadaye wanaishia kuja kuumbuka, kwani kuna haja gani kutufanyia hizi show off hata kama ndiyo nyumba yake mpya?” alihoji jamaa aliyejiita Kitoo kwenye Instagram.

 

Kama hiyo haitoshi, jamaa huyo alizidi kufunguka kuwa kwa namna yoyote ile Mobeto hawezi kuepuka kuhusiana na suala zima la picha zake kusambaa kwani watu waliozivujisha ni watu wake wa karibu ikiwemo akaunti inayojulikana kama mobettohtothetop.

“Ni show off tu hizi wanapenda kutuletea ambazo hazina maana yoyote halafu baadaye utakuja kukuta ata si yeye aliyepanga, utakuta nyuma kuna mwanaume,” alisema.

 

Amani lilipata nafasi ya kuzungumza na mtu wa karibu na Mobeto ambaye alisema hata hajafurahishwa na Mobeto anavyofanya show off ambazo mara nyingi zinakuja kumtukanisha yeye pamoja na timu nzima inayomuunga mkono.

 

“Unakumbuka kipindi kile cha lile gari alilojizawadia wakati wa bethidei yake, sisi mashabiki wake tuliamini ni lake lakini mwisho wa siku ikaja kubainika ni la dalali mmoja maarufu wa magari,” alisema mtu huyo huku akiomba hifadhi ya jina.

 

Gari hilo lilizidi kuleta tafran mitandaoni baada ya baadaye mama Mobeto, Shufaa Rutiginga kutofautiana kauli na mwanaye.

Mobeto alisema amejizawadia lakini mama yake alipohojiwa na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, alisema bintiye amepewa zawadi na mtu ambaye hakupenda kumtaja jina.

 

Gari hilo lilikuja kubainika pia liliwahi kukodiwa na muigizaji Mwijaku na kupiga nalo picha. Picha hizo zilivujishwa kwenye mitandao na kuzua gumzo kama lote.

Mtu huyo alizidi kumwaga ubuyu kuwa, mbali na hilo la gari, alikumbushia nyumba ambayo alipangiwa na mzazi mwenziye Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ maeneo ya Bahari Beach jijini Dar.

 

“Angalia pale tuliumbuka baadaye maana sisi wapambe tulibeba tu kwamba nyumba ni yake kanunua, baadaye tukaambiwa kanunuliwa na Diamond baadaye ikaja kufahamika hajanunuliwa wala nini bali alipangiwa na Mondi,” alisema mtu huyo wa karibu na Mobeto.

 

Mwishoni alimtaka Mobeto kujaribu kuyafanya maisha yake kuwa ya siri na hamna sababu ya kujitangaza pindi anapohamia katika nyumba au kununua gari jipya maana baadaye inakuja kubainika ndivyo sivyo halafu wanaoumia ni wao.

 

“Tunaoumia ni sisi. Tunatukanwa sana mitandaoni baada ya kujimwambafai kama nyumba ni yake halafu baadaye inabainika si yake au gari fulani ni lake halafu kumbe si lake,” alisema.

 

Hata hivyo licha ya mtu huyo kusema hayo, Mobeto mpaka sasa hajaweka wazi kama mjengo huo mpya aliohamia hivi karibuni ni wake kwa kuumiliki au amepangisha.

Amani linafahamu kuwa tayari Mobeto amehamia kwenye nyumba hiyo lakini lilipojaribu kumvutia waya ili kuweza kujua nyumba ni yake au amepanga, simu iliita bila kupokelewa

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Leave A Reply