Kuisapoti Yanga Kutaifanya Ipate Ushindi Leo

TIMU ya Yanga inacheza mchezo wake wa pili leo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Huu ni mchezo muhimu sana kwa maendeleo ya soka letu,  lakini ni mchezo wa kitaifa kwa kuwa Yanga inawakilisha Tanzania nzima na siyo klabu yao tu.

 

Nafikiri leo ni siku muhimu sana kwa Yanga kupewa sapoti na Watanzania wote bila kujali kuwa ni mashabiki wa Simba, Yanga, Azam au wa timu nyingine yoyote ile.

 

Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa timu hii inapata sapoti ya kutosha, mara nyingi kumekuwa na hali ya kukata tamaa kuwa Yanga hawawezi kufanya jambo lolote kwenye mchezo wa leo, lakini ukweli ni kwamba kama wakipewa sapoti wanaweza kufanya maajabu na kuibuka na ushindi mnono.

 

Kuna nafasi ya Yanga ya kufanya vizuri kama itafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yake iliyobaki hapa nyumbani.

 

Ni jambo zuri kama Watanzania wote tutakuwa kitu kimoja kuhakikisha kuwa timu hii inafanya vizuri leo, twende uwanjani kwa wingi na kuisapoti timu hii kwa nguvu kubwa kwa kuwa inapeperusha bendera ya taifa.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment