The House of Favourite Newspapers

Kukopi Na Kupesti Hakutaiacha Salama Bongo Fleva

0
Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

NYIMBO nyingi za Bongo Fleva kwa sasa zinabebwa na ubora wa video ambayo msanii anai­fanya. Hapa unaweza kukuta wimbo wa kawaida ambao hata haueleweki lakini inatumika gharama kubwa kuhakikisha video yake inakuwa ya kiwango kikubwa.

Suala hilo limewafanya wasanii wengi Bongo kufukuzana na hali hiyo, jambo ambalo limesababisha baadhi yao kuchukua mawazo ya video za wasanii wenzao na kuyaingiza kwenye video zao, yaani kukopi na kupesti.

Awali, suala hilo lilianza kama utani hivi lakini kwa sasa limejichimbia miz­izi na kukomaa. Idadi ya wasanii ambao wanapesti mawazo ya wenzao katika video zao ni kubwa kuliko kipindi cha nyuma.

Mwanzoni kabisa gazeti hilihili la Cham­pioni, liliibua na kuonyesha jinsi msanii Dia­mond alivyorudia mawazo ya wasanii wen­gine hasa wale wa Ulaya kwenye video ya nyimbo zake. Alianza na Make Me Sing kisha Kidogo na sasa kamal­izia na Fire ambayo video yake in­afanana na ile ya Jason Derulo iit­wayo Swalla.

Baada ya msanii huyo kuyafan­ya hayo, hivi karibuni mwanada­da anayekimbiza kwenye game ya muziki huo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ naye kaamua kupi­ta mulemule yaani kakopi kisha kupesti katika mkwaju wake mpya wa Kisela ambao am­empa shavu pacha wa Kundi la P-Square, Paul Okoye.

Kisela ya Vee Money in­afanana na ile ya Energy iliyofanywa na Keri Hilson wa Marekani, lakini tofau­ti ni miaka, wakati Kisela haina hata wiki mbili tangu iachiwe yaani Ju­lai 10, mwaka huu, En­ergy ya Keri sasa inagota mwaka wa nane tangu iachiwe kwake Desemba 13, 2009.

Championi Jumatatu linakuletea baadhi ya maeneo ambayo Vee Money aliyesikika kisanii kupitia Ngoma ya Closer, ameiga kutoka kwenye video ya Energy.

Keri Hilson – Energy

MAZINGIRA YA VIDEO NZIMA

Hapa ndipo tatizo la kukopi na kupesti alilofanya Vee Money linapoanza, haihitaji elimu ya chuo kikuu kutambua kwamba mazingira ya vid­eo zote mbili yanafanana yaani ile ya Kisela na En­ergy.

Vee Money ametem­belea mawazo ya Keri Hilson ya kutengeneza video katika mazingira ya ‘gym’ (sehemu ya ku­fanyia mazoezi kwa wana­masumbwi) ambapo mwanzo mwisho video hiyo imeshutiwa eneo hilo kama ilivyo ya Energy.

UWANJA WA NGUMI

Hili pia ni eneo lingine ambalo Vee Mon­ey ‘dizaini f’lan amelipestisha’ kwenye vid­eo yake ambapo mwanzoni tu mwa video yake anaonekana yuko kwenye ulingo wa ngumi jambo ambalo hata Keri amelifanya katika video yake na hata kukaa kwenye viti vinavyowekwa kwenye kona ya mabondia.

Ukifuatilia kwenye video zote mbili ya Keri na Vee Money, utabaini kuwa wasanii wote wametumia eneo la ulingo kwa asil­imia kubwa katika kushutia video zao.

Msanii wa Kimataifa, Keri Hilson.

KUPIGA PUNCHING BAG

Vee Money ameendelea kuonyesha kuwa hakutumia nguvu kubwa kuwaza kuitengeneza video yake hiyo hata kama atakuwa ametumia fedha nyingi kuiten­geneza.

Eneo lingine ambalo linamuonyesha Vee Money amekopi na kupesti ni kwenye kipengele hiki ambapo kule kwa Keri anaonekana kupiga ‘punching bag’ kwa ajili ya kujiandaa na pambano lake jambo hilohilo linafanywa na Vee Money kwenye video yake ya Kisela. Hapo utaona kabisa kuwa amekopi tu tukio la mwenzake kisha kulihamishia kwake.

KUPIGA SPEED BAG

Kukopi kamwe hakutamuacha salama Vee Money kwani vipengele alivyovitumia kwenye wimbo wake ndivyo vinamhukumu mwenyewe, ukiitazama vizuri Video ya En­ergy kuna sehemu inamuonye­sha Keri akipiga ‘speed bag’ na ukirudi kwa Vee Money naye mwan­zoni alikuwa aki­fanya hivyo kabla ya baadaye kuja kufundishwa na Paul Okoye jin­si ya kukitumia kifaa hicho.

MAKALA: SAIDI ALLY | CHAMPIONI JUMATATU

Leave A Reply