HALOOOOO eeeh shoga yangu mwenzako namshukuru Jalali kwa kunijalia uzima ulioniwezesha kuonana nawe katika uga wetu huu tunaozungumzia ishu za chumbani zaidi au nakoseaaa! Baada ya wiki iliyopita kuwazungumzia wenzetu wanaoishi kama wapo dunia ya kwao, wao chumba wanakiacha kama kilivyo, yaani usafi unakuwa shida! Mwanamke mtu mzima ukimuona msafi kuanzia kucha hadi miguu nenda chumbani kwake sasa kama hujatemea mate chini! Heee heeeiyaaaa!
Shoga mjini ujue kupaka wanja tu kila mwanaume atatamani kukuoa, upo nyonyo? Ona sasa hadi nimesahau kuwaambia kile ambacho kimenileta kwako kwa siku hii ya leo! Leo nipo na hawaa wanawake wenzangu ambao kwao bila kutoka nyumbani hawawezi, mara utasikia nakwenda kwa dada Tatu Kimara, kwa shangazi Kitunda na kwenye kicheni pati Buruguni. Kama wazazi wao wako Chanika na wao wanaishi Mbagala basi haiishi wiki bila kwenda huko, yaani wao ni safari kwa kwenda mbele na kusahau kabisa wajibu wa kutulia nyumbani.
Shoga, ndiyo maana nikaanza na kuku hakanyagi marumaru, kwanza atapoteza uelekeo upo? Sasa kwa tabia hiyo ya kila kukicha wewe ni kiguu na njia lazima mumeo atakutilia shaka na kwa ambaye hataki kupiga kelele lazima atatafuta mchepuko tu!
Atafanya hivyo kwa sababu kila akirudi nyumbani akitegemea utampokea, utampa pole ya kazi, utamwandalia maji ya kuoga na chakula, anaambulia patupu,wewe haupo. Shoga yangu, kwa tabia hiyo ni rahisi mumeo kutokukuamini na kuhisi unamsaliti na mbaya zaidi ni pale inapotokea kila ukitoka nyumbani simu yako haipatikani hewani.
Kwa wewe mwenye tabia hiyo, unapaswa kuelewa kwamba heshima ya mwanamke ni kutulia nyumbani, hata unapotoka iwe kwa safari za muhimu lakini siyo kila kukicha wewe ni kiguu na njia. Kwa leo niishie hapa nisije kuonekana muongeaji sana bureee! Ni mimi Anti Naa ukipenda waweza kuniita Shangingi Mstaafu.
Comments are closed.