The House of Favourite Newspapers

Kuku Wamuokoa Timbulo

MSANII wa Bongo Fleva, Ally Timbulo ameweka wazi kwamba, kilichomuokoa kwenye maisha ukiachana na muziki ni ufugaji wa kuku ambao mpaka sasa umemfanya asitegemee pesa za shoo kama wasanii wengine.

 

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Timbulo alifunguka kuwa, aliamua kujishughulisha na mambo ya ufugaji baada ya kuona hawezi kukaa tu na kusubiria shoo maana kuna wakati zinakata kabisa hivyo hata pesa ndogondogo inakuwa ni shida.

 

“Nina kuku 2,000 ambao nafuga na nina wauza kwa bei tofauti. Kuna wengine wanaanzia elfu 15 hadi elfu 40 kutegemeana na mbegu. Pia ninauza mayai, inanisaidia mimi na familia yangu,” alisema Timbulo ambaye hivi karibuni aliachia Ngoma ya Sangoma.

Imelda Mtema

Huyu Ndiye Mshindi wa Miss Tanzania 2018

Comments are closed.