The House of Favourite Newspapers

Kula Mayai Kunaweza Kukusababishia Kifo

 

WATAALAM wamekuwa wakiumiza vichwa kwa miaka kadhaa iwapo ulaji wa mayai ni mzuri au mbaya kwa afya yako.

 

Yawezekana jawabu la swali hilo linategemeana na mayai mangapi unakula kwa wiki – hayo ni kulingana na utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la jumuiya ya matabibu wa Marekani (JAMA).

 

Kwa mujibu wa jarida hilo, kula mayai mawili tu kwa siku kunaweza kusababisha magonjwa ya moyo na hata kifo cha mapema.

 

 

Hilo linatokana na kiwango kikubwa cha kolestro kinachopatikana kwenye kiini. Yai kubwa moja linakuwa na mpaka miligramu 185 za kolestro kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Marekani – zaidi ya nusu ya kiwango cha kolestro ambacho Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri mtu ale kwa siku ni miligramu 300.

 

Utafiti wa JAMA ulichakata taarifa kutoka katika majaribio sita yaliyohusisha zaidi ya watu 30,000 katika kipindi cha miaka 17.

 

Watafiti wamefikia hitimisho kuwa kula miligramu zaidi ya miligramu 300 za kolestro kwa siku kunaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa 17% na vifo vya mapema kwa 18%.

 

Uwiano huo wa hatari huongezeka zaidi kwenye ulaji wa mayai, na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo kwa ulaji wa mayai, na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo kwa 6% na vifo vya mapema kwa 8%.

 

 

Kwa mujibu wa utafiti huo, madhara hayo ya mayai hayaathiriwi na umri, nguvu ya mwili, matumizi ya tumbaku na historia ya kuwa na shinikizo la damu.

 

“Utafiti wetu umebaini kuwa, endapo watu wawili watafuata aina moja ya mlo ya aina moja na tofauti pekee ikawa ni ulaji wa mayai, basi yule ambaye mwenye kula mayai mengi ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya moyo,” anasema Norrina Allen, Profesa mshiriki wa madawa ya kinga katika Chuo Kikuu cha Northwestern University na mwandishi wa utafiti.

 

Utafiti mpya unatofautiana na kazi za tafiti za awali ambazo zilibaini kuwa hakuna uhusiano kati ya ulaji wa yai na uwezekano wa hali ya juu wa kupata magonjwa ya moyo.

 

Lakini Allen anasema kwamba hizo zilikuwa na sampuli tofauti chache na zilikuwa na muda mfupi wa kufuatilia walaji wa mayai.

 

Hata hivyo, watafiti wanakiri kuwa huenda kuna makosa katika uchunguzi wao. Data kuhusu ulaji wa yai zilikusanywa kwa njia ya maswali ambapo ilibidi walioulizwa kukumbuka chakula chao katika kipindi cha miezi na miaka

 

Watafiri wengine pia walisema kuwa matokeo ni ya kuchunguzwa na ingawa walieleza uhusiano kati ya ulaji wa yai na kuongezeka kwa hatari ya ugonjwa wa moyo na kifo cha mapema, hawawezi kuthibitisha sababu.

 

“Umuhimu wa utafiti huu ni kwamba uliwakilisha jamii tofauti za watu wa Marekani na chakula kinacholiwa na Wamarekani wa kawaida ,” anasema Tom Sanders, profesa wa masuala ya lishe katika taasisi ya King’s College mjini London akiongeza kwamba ukomo wake unategemea kipimo cha ulaji wa lishe moja.

 

Inapendekezwa kula mayai japo matatu kwa muda wa wiki moja na inapaswa kula sehemu ya nje nyeupe ya yai zaidi kuliko kiini cha rangi ya njano

Comments are closed.