The House of Favourite Newspapers

Kulegea kwa misuli sehemu za siri za mwanamke (Vaginal Prolapse)

Wanawake wengi wenye umri mkubwa hupata maradhi ya Vaginal Prolapse yaani kulegea kwa misuli ya uke au sehemu za siri za mwanamke ambapo uke hutanuka zaidi ya kipenyo chake cha kawaida ambacho ni sentimita nne.

Licha ya wanawake wenye umri mkubwa pia wasichana wanaweza kupata ugonjwa huu. Tufafanue kuwa kulegea kwa misuli ya uke kuna tofauti kidogo na kutanuka kwa misuli hiyo.

Misuli hiyo inapolegea huwa inashindwa kubana na kuachia njia lakini inapolegea mgonjwa akichuchumaa huhisi nyama kujitokeza nje ya uke.

Dalili

Dalili kubwa ni mwanamke anapojishika au kujisafisha ukeni anahisi kuziba kwa tundu kutokana na kujaa nyama iliyotoka ndani. Pia mwanamke atakuwa akijisikia muwasho na uchafu sehemu za siri na hasa wakati wa kujamiiana.

Dalili nyingine ni mgonjwa kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa na hali hiyo itatokea kutokana na michubuko. Mara nyingi hali hiyo ya kuziba kwa njia ikitokea mwanamke hawezi kujisikia kufanya tendo la ndoa, hii ni kwa sababu atakuwa ana michubuko sehemu zake za siri.

Michubuko hiyo itakuwa inamfanya mwanamke mwenye tatizo hilo kupata maambukizi mbalimbali ambayo huweza kufika kwenye mlango wa uzazi au tumbo la uzazi au kwenye mirija na vifuko vya mayai, hivyo kusababisha aumwe na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara.

Lakini pia mwanamke huyo atakuwa na tatizo la mwenendo wa siku za hedhi kuvurugika hivyo kukumbwa na tatizo la kupata ujauzito. Hali hiyo ya kulegea kwa uke ikimkumba mwanamke huathiri mume au mpenzi wake wakati wa tendo la ndoa.

Itaendelea wiki ijayo.

Comments are closed.