Michael Cohen akiri kumwibia Donald Trump dola 60,000
Michael Cohen, aliyekuwa mshirika wa kisiasa wa Donald Trump, alikiri siku ya Jumatatu kuiba dola 60,000 kutoka kwenye utajiri mkubwa wa biashara za nyumba za rais aliyekuwa akitarajiwa kwa sababu alihisi Trump alikuwa amemlaghai kuhusu kiwango cha bonasi yake ya mwisho ya mwaka 2016.
Kukiri kwa Cohen kulikuja wakati akitoa ushahidi kwa saa kadhaa katika kesi ya jinai ya Trump huko New York. Wakili wa utetezi wa Trump Todd Blanche alimuuliza Cohen ya kumlenga. Baadaye, mwendesha mashtaka Susan Hoffinger alitaka kurekebisha sura ya Cohen mbele ya jopo la mahakama la watu 12 kwa kumuuliza maswali yaliyolenga kufafanua majibu ya Cohen chini ya uchunguzi wa wakili Blanche ambao ulichukua siku tatu.
Blanche alishambulia uaminifu wa Cohen, ambaye kwa miaka mingi alifanya kazi kushughulikia kila mahitaji ya Trump kabla ya kumgeuka mwaka 2018. Cohen, shahidi muhimu zaidi wa mwendesha mashtaka, wiki iliyopita alikubali kwamba kwa miaka mingi amekuwa akidanganya kwa niaba ya Trump na. hiyo ilijitokeza tena katika ushuhuda wake wa Jumatatu.
Wizi wa pesa hizo kutoka kwenye Shirika la Trump, Cohen alikiri, ulichangia sehemu kuu ya kesi dhidi ya Trump, ambaye amekanusha mashtaka 34 yanayomkabili. Trump ndiye mgombea mtarajiwa wa urais wa chama cha Republican kwa mwaka 2024 dhidi ya Rais Joe Biden, Mdemocrat ambaye alipata ushindi dhidi ya Trump mwaka 2020.