The House of Favourite Newspapers

Kumbe Iyobo hakummisi kabisa Aunt

0

DANSA kiwango ndani ya Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo amefunguka kuwa hakuwahi kummisi mzazi mwenziye ambaye ni staa wa Bongo Muvi, Aunt Ezekiel kwa sababu alikuwa na mpenzi mwingine.

Akizungumza Risasi Mchanganyiko, Iyobo alisema kuwa kitu kikubwa alikuwa anammisi mtoto lakini mzazi mwenziye huyo alimtoa kichwani kwa sababu alishamuanika mpenzi mwingine kwenye mitandao.

“Sikummisi kabisa, sababu kubwa tayari alikuwa na mpenzi mwingine ambaye alikuwa akimposti kwenye mitandao. Mimi nilimmisi Cookie tu,” alisema Iyobo. Wawili hao walimwagana kwa miezi kadhaa lakini sasa wamerudiana na penzi lao ni ‘shata shata’.

Stori: Imelda Mtema

Leave A Reply