The House of Favourite Newspapers

Kumbe Kajala Watammisi Sana!

KILA kitu kina wakati wake! Hebu msikie staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’, anasema eti kwa jinsi ambavyo haonekani hovyo sehemu mbalimbali, siku zinavyokwenda ndiyo hawatamuona na watammisi kinoma.

 

Kajala ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, ifike mahali mtu akue na kubadilika na hicho ndicho kilichotokea kwake kwani kwa sasa anaweza kukata hata mwaka bila kuonana na mastaa wenzake.

 

“Unajua muda unavyosonga ndivyo mambo yanabadilika, hicho ndicho kilichotokea kwangu na kweli watu watanimisi sana. Mambo ya mjini sasa hivi tumewaachia wasichana kama akina Paula (mwanaye),” alisema Kajala.

STORI: IMELDA MTEMA,DAR

Comments are closed.