The House of Favourite Newspapers

Kumbe Martin Kadinda ngangari

0

Kadinda-3.pngRichard bukos, Amani

Dar es Salaam: Mwanamitindo wa kiume Bongo, Martin Kadinda amenaswa akiwa ngangari akimbambia kimahaba kimwana ambaye jina halikufahamika mara moja hivyo kuibua minong’ono kuwa kumbe naye hayupo nyuma kwenye matukio kama hayo tofauti na alivyozoeleka kuwa siyo mtu wa kujirusha na ‘totoz’.

Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mlimani City uliopo Barabara ya Sam Nujoma jijini Dar kulipokuwa na ile Shoo ya Naamka Tena ya Mwana-muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’.

Katika tukio hilo, Kadinda ambaye ni Meneja wa Mwigizaji Wema Isaac Sepetu aliingia ukumbini humo akiwa amemu-weka kushoto mrembo huyo huku akikishikilia kiuno chake.

Mikogo yao haikuishia hapo kwani hata walipokuwa wakienda maliwatoni, walisindikizana kwa staili hiyohiyo na kuwaacha watu macho kodo.

Kuonesha kama ‘walipania’, waliposikia Wimbo wa Ndi Ndi Ndi wa Jide ukipigwa, walivamia sehemu ya kuchezea (dance floor) na kuanza kusakata muziki wakiwa ziro distansi.

“Jamani leo (usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita) namuona

 Kadinda yupo ngangari na kitu chake (mrembo), amekomaa, hataki mchezo asije akanyang’anywa tonge mdomoni,” alisikika mmoja wa mashabiki wa Ndi Ndi Ndi ya Jide.

Hata hivyo, Amani lilimnyatia Kadinda na kumuuliza kulikoni au mrembo huyo ndiye waifu wake ambapo aling’aka:

“Acheni umbeya wenu bwana….Tuacheni tule raha zetu.”

Leave A Reply