The House of Favourite Newspapers

Kumbe Mchumba wa Ngwea Alisepa Zake!

Miaka sita baada ya kifo cha aliyekuwa staa wa muziki wa HipHop Bongo, Albert Mangweha ‘Ngwea’, imeelezwa kuwa aliyekuwa mchumba’ke, Misheily, raia wa Ufaransa alisepa miaka miwili baada ya kifo hicho.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, mama mzazi wa Ngwea, Denisia Magweha alisema kuwa, aliishi vizuri mno na Misheily, lakini tangu alipoondoka hakurejea.

“Tuliishi vizuri sana na Misheily, alikuwa akinifariji sana na alikuwa na roho nzuri sana.

“Alipoondoka alisema angerejea na kweli alikuwa akiwasiliana vizuri na dada zake Albert (Ngwea).

“Lakini baadaye mawasiliano yalikatika na hatujui yupo wapi, kama anaweza kupata taarifa, ajue tu kwamba tunamkumbuka, tunaamini kuna siku atarejea,” alisema mama Ngwea na kumaliza maswali juu ya alipo Misheily.

 

Ngwea aliyekuwa mkali wa freestyle Bongo alifariki dunia Mei 28, 2013 huko nchini Afrika Kusini ambapo kifo chake kiliibua utata mkubwa.

Stori: DUNSTAN SHEKIDELE, IJUMAA | Morogoro

Comments are closed.