Kumbe Nandy Yupo Kwenye Tuzo za Grammy

HII ni hatua nyingine kubwa kwa msanii Nandy kwenye safari ya kuelekea katika Tuzo za Grammy siku za usoni.
Hii ni kufuatia Nandy kuwepo kwenye tuzo hizo kupitia albam ya pamoja ya msanii Etana wa Jamaica ambayo imeingia kwenye kuwania Tuzo za Grammy 2022.
Ndani ya albam hiyo, Nandy ameshirikishwa kwenye moja ya nyimbo zinazopatikana ndani yake.
Albam hiyo yenye jina la Pamoja imeingia kwenye tuzo hizo katika Kipengele cha Album Bora ya Reggae (Best Reggae Album).
Nandy amesema; “Ninayo furaha kubwa sana kuwa miongoni mwa wasanii walioshirikishwa kwenye album iliyochaguliwa kwenye Tuzo za Grammy 2022…”
STORI; SIFAEL PAUL, DAR

