HE! KUMBE SHEPU YA SANCHI SIRI NI MADAFU!

Jane Ramoy ‘Sanchi’

WAPO wanawake wanaotamani kuwa na shepu kama ya mwanamitindo Jane Ramoy ‘Sanchi’ lakini mwanadada huyo ameanika siri ya muonekano wake.  

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Sanchi alisema kuwa, madafu yana mchango mkubwa sana kwenye shepu yake kwani hupendelea kunywa maji yake badala ya maji ya kawaida au kimiminika kingine.

 

“Mimi nitawapa siri yangu leo, madafu ndio kila kitu kwangu na hii tangu niko mdogo. Mama alikuwa akipenda sana kunywa maji ya madafu, nikawa namuuliza kwa nini? Ndiyo akaniambia ni siri ya kuwa mrembo.

“Kuanzia wakati huo kila nikisikia kiu, l abda dafu lisiwepo lakini likiwa lipo karibu maji yake ndiyo ya kuniondolea kiu, najua pia yananifanya nionekane mrembo zaidi,” alisema Sanchi.

 

Mwanadada huyo anatoa elimu kuwa, maji ya madafu yanafanya tumbo kuwa na mfumo mzuri kwa sababu yanasafisha kila kitu, hadi mkojo unakuwa safi.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment