The House of Favourite Newspapers

Kumlea mwana kunahitaji maandalizi, usijizalie tu

0

pregnant-black-womanAsalam alaikum wapenzi wasomaji wangu, bila shaka ni wazima kwa wakazi wa Dar poleni na hali ya hewa kwani kila ninayekutana naye analalamikia joto kali ambalo wengine linawaathiri.
Tuzidi kumuomba Mungu joto hili lipungue badala ya kuongezeka kwani ni hatari, baada ya hayo turejee kwenye mada yetu ya leo nia ni kuwaweka sawa akina mama wenzangu ambao hawajui mafunzo ya malezi.
Utakuta mwanamke anaamua kuzaa  kila baada ya miezi tisa na wala hafikirii kuhusiana na malezi yeye anaona sawa tu, unajua linapokuja suala la kuzaa anayelaumiwa ni mama anayezaa si baba na matunzo yakiwa mabaya anayelaumiwa sana ni mama sasa hili mlijue wanawake wenzangu.

Kum-buka anaye-takiwa kupanga uzazi na akaweza ni wewe mwanamke baba hatakiwi kujihusisha sana na hilo kwani ana mambo mengi ndiyo maana unapokuwa na watoto wengi watu wanakushangaa wewe siyo baba.
Sasa basi mada ya leo inasema kulea mwana kunahitaji maandalizi kwa maana hii ukiamua kuwazaa watoto panga na jinsi utakavyowalea kwa maana ya malezi bora kwa ujumla.

Wazazi wa siku hizi wanawalea watoto wao kwa kutegemea wafanya kazi wa ndani hivi mfanyakazi akulelee mtoto atakuwa mtoto kweli na wengine wanajiachia hivyo kwa sababu hawawezi kuwalea watoto waliofuatana.
Ujauzito wa kwanza hakikisha unarudi kwenu kwa mafunzo zaidi.

Wanawake wengi wakishaolewa siku hizi wanautupilia mbali utamaduni wa mila na desturi zetu ambao humlazimisha mwanamke kurudi nyumbani kwao kwa ujauzito wa kwanza kwa ajili ya mafunzo ya uzazi.
Huko utajifunza mtoto umfuatishe akiwa na umri gani, utajifunza malezi yapi yanayotakiwa, unajua wakati mwingine unaweza kupata mtoto akawa ni wa kuuguaugua na usijue la kufanya.

Huko kwenye mafunzo utafundishwa nini cha kumfanyia mwanao asipatwe  na magonjwa ya mara kwa mara, vitu hivi si rahisi kufunzwa ukweni unatakiwa kujifunza nyumbani kwenu ambapo hawatakuonea aibu.
Nimeamua kuandika mada hii kwa sababu ndoa nyingi zinavunjika kisa akina baba kuwalaumu wake zao kwamba wanapenda kuzaa bila mpangilio wakati si kweli.

Familia kuongezeka ni mpango wa baba na mama si mama peke yake kwa sababu linapokuja suala la malazi ukiacha malezi baba anahusika kwa asilimia kubwa.
Baba Juma wa Manzese aliniambia amefikia hatua ya kumbeba mkewe kumpeleka kufunga kizazi kwa sababu haelewi uzazi wa mpango, nikamhoji kama amewahi kumkubalia kwenda nyumbani kwao akiwa mjamzito? Akasema hapana.

Hiyo ni shida akina baba wengi wamekuwa wakiwabana wake zao na kuhisi kwao kutabadili ndoa yake lakini kuna mambo ambayo huwezi kuyafumbia macho na inapendeza mtu kufundishwa pale anapokuwa tayari ana mfano wa kuongelea.
Hili bila shaka ni funzo kwa akina baba naomba liwaingie na mlipe kipaumbele kwani hata uwe umejifungua watoto sita ukibeba wa nane ushasahau kila kitu unatakiwa kukumbushwa

Leave A Reply