The House of Favourite Newspapers

Kumradhi DC Sofia Mjema

0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sofia Mjema.

NA MHARIRI WA GAZETI LA IJUMAA

NDANI ya gazeti hili, toleo namba 1038 la Mei 1925, 2017 katika ukurasa wa mbele kulikuwa na kichwa cha habari kilichosomeka; ‘Mkuu wa Wilaya aanika maisha yake ya kimapenzi.

Hiyo ilitokana na mahojiano maalum yaliyofanyika kati ya Mheshimiwa Sofia Mjema ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala na mwandishi wetu, hatimaye kumuandikia makala iliyokuwa inazungumzia maisha yake kuanzia alipokuwa shule ya msingi mpaka alipo sasa.

Hata hivyo, katika mahojiano hayo, kuna mambo ambayo mheshimiwa huyo aliomba yasiandikwe gazetini kwa sababu maalum lakini kwa kupitiwa, yalipenya baadhi ya mambo ambayo baada ya gazeti kutoka yalileta usumbufu mkubwa kwa kiongozi huyo.

Sisi ni binadamu, hatukuwa na dhamira mbaya na tunakiri kuna kosa limefanyika sehemu, hivyo tunachukua nafasi hii kumuomba radhi Mheshimiwa Mjema na watu wake wa karibu kwa usumbufu waliopata na tunaahidi kwamba tutaongeza umakini zaidi katika kazi zetu siku zijazo. Mhariri.

Leave A Reply