visa

Kumsifia mume/ mkeo kwa marafiki unakosea!

vegeterians-couple-bedKAMA kawaida ni siku nyingine tena tunakutana katika kujadili mada za kuhusu maisha yetu ya kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Yapo mambo mengi yanayotokea kila siku katika maisha ya mapenzi, mambo hayo yanawezekana kuwa ni ya lazima kutokea, unayasababisha mwenyewe au unaruhusu yatokee bila ya sababu.

Kutokana na hayo yote, leo nitazungumzia baadhi ya wapenzi wenye tabia za kutoa mambo ya faragha na kuyapeleka kwa mashoga au rafiki zao.

Kila unachokifanya usiku, mchana au asubuhi na mpenzi wako, basi mama au baba wa jirani anafahamu, mkikwaruzana kidogo, ukimnyima mwenzio haki yake ya ndoa, basi mama au baba mwenye nyumba anajua kila kitu kilichotokea.

Sidhani kama ni sawa, hili ni tatizo ni moja ya upungufu mkubwa katika uhusiano, sasa utofauti wenu mkiwa mmevaa na mkiwa watupu uko wapi ikiwa kila kitu unaenda kukianika kwa rafiki zako?

Unadhani yeye hapendi vitamu na vizuri au raha kama ambazo umekuwa ukimsimulia? Unadhani yeye hapendi raha na ujuzi ndani ya sita kwa sita!

Usitengeneza mazingira ya kumshawishi mtu dhidi ya mpenzi wako, ya chumbani yabaki kuwa ya chumbani na ya sebuleni yawe ya sebuleni, pia ya kijiweni au saluni yaishie huko huko. Usichanganye ya chumbani na sebuleni au saluni kuwa sehemu moja, utakuwa umeharibu sana.

Kama kuna kosa kubwa ambalo ulikuwa hulijui linaweza kukumaliza kwenye uhusiano basi ni mwanaume au mwanamke kuwasimulia rafiki zake kuwa mumewe au mkewe anayaweza mambo fulani au ana upungufu fulani.

Kwanza inashangaza sana unawezaje kusimulia mambo nyeti kiasi hicho, mambo ya faragha ni siri kama ilivyo usalama wa taifa, ndivyo ambavyo unapaswa kuiona kuwa ni sekta nyeti sana.

Kwa kweli inasikitisha kuona kila unachofanyiwa na mpenzi wako unakwenda kuwaambia mashoga zako. Eti, ooooh! Jana bwana’angu kanifanyia hivi, kanigeuza hivi, kiukweli usiku wa jana nimeinjoy sana kwa penzi la mpenzi wangu, nashukuru Mungu nimempata mpenzi anayeyajua mambo, kwa hilo sina shaka kabisa.

Tabia hii ipo kwa pande zote mbili, wanaume kuhadithiana na hata wanawake pia kufanya hivyo, lakini siyo wote. Unakuta kijana yuko kijiweni na washikaji zake kakazana kuwasimulia wenzake, Mwajuma ni mjuzi faragha, anajua kuzungusha nyonga hakuna mfano wake, mwanangu yaani nashindwa namna ya kuelezea wewe elewa mambo anayaweza.

Itaendelea…

Kwa ushauri na maoni tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Ista:mimi_na_uhusiano au jiunge kwenye group letu la WhtsApp kwa namba iliyopo juu.
Toa comment