The House of Favourite Newspapers

Kuna Dalili Faiza Kupigwa Mimba Nyingine!

MACHUNGU yote yameondoka kwa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Faiza Ally baada ya kutumia muda mrefu na baba wa mtoto wake wa pili aitwaye Li huku akisema kuwa kuna kila dalili akapigwa mimba nyingine.

 

Faiza ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, ‘amespendi’ muda mrefu na mzazi mwenzake huyo tangu atue Bongo akitokea China na kusema kuwa akinasa ujauzito atakuwa amefanya jambo kubwa kwenye mapumziko yao.

 

“Kama nitatoka salama bila kupigwa mimba sijui, maana nilikuwa kwenye fungate ya maana na kilichokuwa kikisomeka kichwani kwangu ni mahaba tu,” alisema Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili.

 

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.