KUNA VIUMBE WA AJABU WAISHIO ANGANI -9


NILIPOISHIA IJUMAA ILIYOPITA;
Wiki iliyopita tuliona jinsi Aliens na UFO vilivyoanza kuonekana kwenye anga la Israel, Iran na Australia kwa wakati mmoja.
SASA ENDELEA…
Baada ya kuonekana sehemu mbalimbali duniani na hata Afrika. Kumekuwa na makundi mbalimbali ya viumbe hawa ambao wanasemekana kuingia mikataba na wanasayansi wa anga kwa ajili ya kubadilishana teknolojia. Mfano ni ile teknolojia ya Aliens Software. Kwa bahati mbaya ni kwamba mikataba yao huwa na masharti mengi mabaya ambayo yanamuathiri na mengine yameshamuathiri binadamu na bado mengine yanakuja.

 

Wapo wasioamini, lakini wengine wanaamini huo ndiyo ukweli. Mwaka 1952 nchini Marekani kuliibuka utani kuwa aliens wametua rasmi ikulu ya nchi hiyo kwa lengo la kuingia mikataba mbele ya rais wa wakati huo. Ndivyo umma ulivyoaminishwa na watu wa propaganda.

 

Pia kitendo cha UFO kuonekana huko Washington, Marekani katika kipindi hichohicho, ndipo watu wakaanza kukubaliana na uvumi uliokuwa umeenezwa kuwa aliens, UFO na wanasayansi wa Marekani walikuwa wana uhusiano.

 

Uwepo wa mawasiliano hayo ulitikisa Marekani ikiaminika kuwa ndiyo mwanzo wa uvamizi wa viumbe hao duniani. Usiku mmoja mnara wa rada ya Uwanja wa Ndege wa Washington ulinasa vifaa visivyojulikana ambavyo vilikuwa vikikatiza angani kwa kasi ya ajabu kisha vikaelekea moja kwa moja kwenye ikulu (Whitehouse) ya nchi hiyo.

 

Wakazi wa jirani na eneo hilo walishuhudia vitu kama baluni za rangi ya njano vikidondoka kutoka angani. Vitu hivyo vilikuwa na mikia. Muda mfupi baadaye rubani mmoja alishuhudia UFO saba zikirandaranda angani. Baadaye anga lote lilijazwa na vitu hivyo vilivyokuwa na mwanga mkali. Vitu hivyo vilishuhudiwa na macho ya watazamaji hivyo ule uvumi sasa ukageuka habari ya kweli.

 

Wakati hayo yakiendelea kuliibuka habari za mauaji ya kimbari huko Amerika ya Kusini. Ilielezwa kuwa mauaji hayo ya kutisha yalifanywa na hawa aliens. Hata hivyo, baadaye ilisemekana kuwa shetani alikuwa ametembelea Amerika ya Kusini. Swali ni je, watu walitambuaje kuwa ni shetani? Ilibidi kurudi kwenye maandiko juu ya uumbaji wa mbingu na nchi ili kujua kama Mungu alimuumba shetani?

 

Biblia inasema kuwa Mungu aliumba malaika wengi sana. Lusifa alipendeza zaidi ya malaika wengine lakini kiburi kilimwingia akaasi. Alifanikiwa kushawishi theluthi moja ya malaika wote na wote walifukuzwa kutoka mbinguni (shetani alianguka kutoka mbinguni kama mwanga wa radi (Luka 10:18).

 

Mbingu ni dunia ya roho (spiritual world) sayari kama Dunia, Mars, Jupiter na nyingine ni ulimwengu wa kuonekana. Kwa kawaida binadamu hawezi kuona dunia ya roho ila akifunguliwa macho ya roho. Hapa duniani tunaongozwa na hisia tano tu (sight, smell, hearing, taste na touch (au feel). Hiyo ndiyo maana binadamu anaongozwa na muda na nafasi.

 

Kwa mfano, huwezi ukapenya kwenye ukuta au kupaa angani kama ndege. Hebu fikiria tu kuwa na uwezo wa kunusa au kuona sauti! Ukisafiri mbali sana na kurudi baada ya miaka kama minne-mitano, mtoto wa kike uliyemwacha mdogo atakuwa amechanuka.

 

Ulipotoka, ulitoka na picha ya huyo msichana mdogo kwenye fahamu yako. Unaporudi, unarudi na picha hiyohiyo kwenye fahamu yako. “Ala! vipi? Amebadilika sana huyu!” Utashangaa. Wanaoishi naye watakushangaa wewe kwani hayo mabadiliko unayoyasema wao hawayaoni.

 

Huo ni mfano wa anaongozwa na muda na nafasi. Wanasayansi wa Marekani wametafuta viumbe wenye uhai (au uwezekano wa uhai) kwenye mwezi na sayari kama Mars lakini hawakufanikiwa. Sasa wanadhani kwamba kunaweza kukawa na uwezo wa uhai au kuishi kwenye mwezi au sayari nyinginezo. Wanasayansi wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakitofautiana juu ni sayari gani hasa inaweza kuwa makazi ya aliens?
Je, ni viumbe gani hawa na wana madhara kiasi gani kwa wanadamu? Tukutane Ijumaa ijayo.
0713 750 910

Loading...

Toa comment