KUNA VIUMBE WA AJABU WANAOISHI ANGANI -2

ILIPOISHIA IJUMAA ILIYOPITA…
Kama tulivyoona Ijumaa iliyopita, wataalam wa anga wanadai kuna viumbe wa ajabu waishio angani ambao hujulikana kwa jina la Aliens.
Kwa mujibu wa wataalam hao, viumbe hawa wako mbali sana kimaendeleo ukilinganisha na binadamu.
SASA ENDELEA…
Baadhi ya watu wananiuliza kwa nini nimeamua kuwaletea simulizi hii na kwamba ina faida gani kuyajua haya?
Lengo hasa la simulizi hii ni kutengeneza kiu ya kutaka kujua juu ya kuwepo kwa ‘wageni’ hao kutoka sayari ya mbali wapo au mahali pengine popote huko angani.

 

Mwaka 1947 aliyekuwa Rais wa Marekani na Freemasons wa Daraja la 33, Harry Truman alitengeneza kile kilichoitwa Majestic 12 au MJ12 ambapo kamati ya siri ya wanasayansi ikishirikiana na serikali ilichaguliwa kulifanyia utafiti na uchunguzi la UFO (vitu vinavyoonekana angani) na viumbe kutoka nje ya Sayari ya Dunia.

 

Richard Hoagland aliyekuwa mzungumzaji wa Umoja wa Mataifa alikuwa na ‘mtu wa ndani’ kutoka NASA (National Aeronautics and Space Administration). Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga ambayo ilianzishwa mwaka 1958.
Jamaa huyo alikuwa akimgewa siri na mambo ambayo NASA hawataki walimwengu wafahamu.
Aliwahi kutoa siri ya kuwepo kwa viumbe hawa na alama kama za piramidi na uso wa mtu kwenye Sayari ya Mars ambazo NASA hawataki watu wafahamu.

Alisema NASA wanaufunika ukweli kwamba wanasayansi wa Marekani wa anga wanao ushahidi juu ya kuwepo kwa viumbe hao na kwamba binadamu (wanasayansi na viongozi wa Illuminati) wameshaanza kuwasiliana na kushirikiana na viumbe hao kwa namna mbalimbali.

Je, ni kweli NASA wana siri juu ya kuwepo kwa ‘wageni’ hao katika sayari yetu au mahali pengine au ni mtumishi anayefanya kazi yake vyema ya kuwapandikiza walimwengu dhana na nadharia kuwa kweli viumbe hao wapo?
Majibu ya utafiti yanasema ni kweli wapo na Serikali ya Marekani huwa haitaki watu wafahamu.
NASA waliwahi kutoa taarifa rasmi za kukataa juu ya kuwepo kwa viumbe hao kutoka nje ya sayari yetu. Walikataa kuwa viumbe hawa hawapo kwenye mwezi wala kwenye Sayari ya Mars.

Hoagland na wenzake waliomegewa habari za ndani wakaja na taarifa kuhusiana na UFO, wageni hao na picha mbalimbali za kwenye mwezi na kwenye sayari ya Mars zinazoelekeza na kuonesha juu ya kuwepo kwa viumbe hao katika maeneo hayo na alama zao, yaani kama vile NASA hawataki walimwengu kufahamu chochote juu ya ukweli huo.

Hoagland na wenzake wana watu wao ndani ya NASA, waliowamegea picha hizo na taarifa zingine, hivyo ‘watu wa ndani’ wanautoa ukweli ambao NASA hawataki watu kufahamu kupitia kwa Hoagland na wenzake.
Hivyo hapa Hoagland anaonekana kama mfichuaji wa mambo ya ndani na mtu mzuri kwa wale wasio na sauti.
NASA wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kufunika ukweli juu ya safari ya kwenda mwezini, tunajua kuna binadamu aliyekanyaga mwezini kupitia teknolojia ya NASA.

 

Hili la NASA wanalifunika walimwengu wasijue, lakini Hoagland na wenzake wanakubali kuwa walikwenda mwezini na kuonesha picha na alama za wageni kutoka mbali zikiwa mwezini ambazo zilipigwa na wanaanga wa NASA walipokwenda mwezini. Sasa Hoagland ni NASA au? Anaonekana kama ni adui namba moja wa NASA na anawapinga NASA na mambo yao ya kufunika ukweli na anakuwa ni tumaini na tegemeo la watu duniani kote kuhusiana na ukweli juu ya UFO na madereva wake. Lakini mwenye jicho haambiwi tazama.

Kama ambavyo kwenye Filamu ya Independence Day, binadamu wote waliunganishwa kupitia majeshi ya nchi mbalimbali kupambana na kitisho kipya kilichojitokeza, kitisho kutoka nje ya sayari yetu.
Usidanganywe na taarifa za kupikwa kisayansi na uwongo juu ya UFO vitu ambavyo vitaonekana ni vitu vya kutisha. Lakini lengo ni kutengeneza adui mwenye nguvu kutoka nje ya dunia (kwa ajili ya kutuunganisha, kwa sasa adui tuliye naye ambaye naye ni wa kutengeneza ni ugaidi. Je, ukwli ni upi? Usikose Ijumaa ijayo.
Simulizi: Sifael Paul: 0713 750 910

KUNA VIUMBE WA AJABU WANAOISHI ANGANI!

Toa comment