Kuna wakati Ebitoke alilia mwenyewe!

UNAFIKIRI kupanda Mlima Kilimanjaro ni kazi lelemama? Sasa taarifa ikufikie kuwa komediani mkali Bongo, Annastazia Exvery ‘Ebitoke’, amejikuta akilia peke yake baada ya kuona uzalendo unataka kumshinda wakati akipanda Mlima Kilimanjaro wikiendi iliyopita.

 

Ebitoke ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, wakati akipanda na wenzake, ulifika wakati akaona hawezi tena kutembea ndipo akaona kuliko kushindwa, ajikaze hivyohivyo huku machozi yakimtoka.

 

“Kupanda Mlima Kilimanjaro ni raha na ni ushujaa, lakini lazima uchanganyikiwe kwanza, maana sikutaka kupitwa, lakini nilipoona nataka kushindwa nililia kama mtoto kisha nikafuta machozi na safari ikaendelea,” alisema Ebitoke aliyekuwa kwenye msafara wa mastaa kibao waliopanda Mlima Kilimanjaro wikiendi iliyopita.

Toa comment