Kundi la Nyuki Lavamia Mahakama Kuu na Kuwashambulia Polisi -Video

Taharuki, waandamanaji na polisi wakitimua mbio.

TAARUKI imeibuka katika viunga vya Jiji la Nairobi baada ya waandamanaji na Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wote kukimbia baada ya kushambuliwa na kundi kubwa la nyuki lililokuwa nje ya Mahakama Kuu nchini humo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano, Septemba 20 wakati Jopo la Majaji wa Mahakama Kuu ya Kenya wakiongozwa na Jaji Mkuu, David Maraga walipokuwa wakitoa hukumu ya kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Rais yaliyompa ushindi mgombea wa Jubilee, Uhuru Kenyatta baada ya kubaini dosari katika mchakato wa kuhesabu kura.

Nyuki walivyotanda.

Kulikuwa na hali ya taharuki wakati kundi la nyuki lilipovamia eneo hilo ambalo lilikuwa limezingirwa na askari wakiwa na magari ya doria. Mmoja wa watu waliokuwepo eneo hilo ambaye ni mlemavu alipatiwa msaada kwa kuondolewa kwa gari la wagonjwa baada ya kujeruhiwa na nyuki hao.

Waandishi wa habari walikuwa sehemu ya waliotimua mbio wakinusuru maisha yao kutokana na uvamizi huo. Kabla ya nyuki kuvamia eneo hilo, baadhi ya wafuasi wa Nasa walisikika wakiwashambulia kwa maneno askari waliokuwa wamezuia barabara kuelekea Mahakama Kuu.

Inadaiwa nyuki walikuwa wameweka maskani karibu na eneo hilo lakini hakuna aliyejua. Kwa mujibu wa taarifa, kelele za waandamanaji ndizo zilizowafanya nyuki kutoka na kuwashambulia.

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO HILO

Toa comment