The House of Favourite Newspapers

Kunguru Watumika Kuzoa Uchafu Nchini Ufaransa

 

BUSTANI ya Puy du Fou katika mkoa wa Vendee magharibi mwa Ufaransa, inawatumia kunguru kukusanya takataka.

Katika mapipa maalum ya taka, kunguru huweka uchafu kwenye kisanduku maalum kwenye pipa.  Uchafu wenyewe ni  vichungi vya sigara au uchafu wowote.  Akishaweka uchafu huo, uzito wake hukifungua kisanduku hicho na kusukumia nje kisanduku kingine kilicho na chakula cha ndege.  Hivyo kunguru hula chakula hicho.

Inasemekana kunguru wana akili ya ajabu na kwamba wakifundishwa wanaweza kumfanyia binadamu mambo mengi ya faida.

 

Comments are closed.