Kartra

Kunta Kinte na Simulizi ya Utumwa Wake Amerika

KUNTA KINTE alikuwa muhusika Katika Riwaya ya “Roots” ya mwaka 1976 mtunzi wake akiwa ni Alex Haley, inasimulia simulizi ya familia ya kiamerika ,kulingana na Haley, Kunta Kinte alikuwa ni mmoja wa mababu zake wa kale, mtu wa nchini Gambia aliyezaliwa mwaka 1750 akatekwa utumwani na kupelekwa Amerika na kufariki mwaka 1822 ,Haley anasema kwamba maisha ya Kunta Kwenye Riwaya ya “Roots” yalikuwa yenye mchanganyiko wa ukweli na kufikirika.

 

Kulingana na riwaya ya Roots, Kunta Kinte alizaliwa mwaka 1750 katika kijiji cha kabila la Mandinka cha Juffure, huko Gambia ,alilelewa na familia ya kiislamu ,siku moja mwaka 1767, Wakati Kunta Kinte anatafuta kuni ili kujitengenezea ngoma kwaajili ya mdogo wake wa kiume ,watu wanne wakaibuka toka msituni na kuanza kumfukuza wakamzidi mbio na kumkamata kama mateka ,alipogutuka toka kwenye usingizi mzito akajikuta amefungwa kitambaa usoni, mdomoni na kamba mwilini kama mfungwa.

 

Yeye na wenzake wakatupwa ndani ya meli ya watumwa “Lord Ligonier” kwa miezi minne wakasafiri kuelekea Amerika kaskazini, Kunta Kinte akaimudu safari ya kuelekea Maryland, alipofika akauzwa kwa bwanashamba huko Virginia aitwaye, John Waller, mmiliki wa mashamba ya spotslvania, ambaye alimbatiza Kinte kwa jina la Toby, jina ambalo Kinte alilikataa pia akagoma kuongea na watumwa wenzake wengine, Baada ya kukamatwa mara kadhaa wakati akijaribu kutoroka kwa mara nne mfululizo ,wale wakamata watumwa wakampa chaguzi mbili achague kukatwa mguu mmoja wa kulia au ahasiwe, akachagua akatwe mguu wake wa kulia wale watu wakamkata mguu ule, miaka iliposonga mbele Kunta sasa akamilikiwa na kaka wa john waller, aliyeitwa Dr. William Waller, akaacha kwa hiari yake matukio yake ya mgomo na kuwa sasa wazi na kuongea na watumwa wenzake lakini hakusahau yeye ni nani au wapi alikotokea.

 

Kunta akamuoa mtumwa mwenzake mwanamke aliyeitwa ,Bell Waller, wakapata mtoto wa kike waliyemwita kwa jina la Kizzy, jina ambalo kwa kilugha cha kina Kunta lilimaanisha “kubakia” alimpa mtoto jina hili kwa makusudi ili asiuzwe mahali pengine. Kizzy alipofika umri wa usichana akauzwa huko Kaskazini mwa Carolina na ni baada ya William Waller kugundua kwamba Kizzy aliandika kibali bandia cha kusafiria cha kijana mtumwa aliyeitwa Noah, ambaye Kizzy alikuwa na mahusiano nae ya kimapenzi. Hiyo ni baada ya Kizzy kufundishwa kusoma na kuandika kwa siri na Missy Anne ambaye alikuwa mpwa wa mmiliki mashamba.

 

Mmiliki wake mpya aliitwa, Thomas Lea, Thomas siku moja akaingia chumbani kwa Kizzy na kumbaka na kisha akampa ujauzito mtoto alipozaliwa alimwita George. Kizzy maishani mwake hakuwahi kujifunza matatizo waliyoyapitia wazazi wake akaishi maisha yake yaliyobakia kama mkulima wa Jembe la mkono katika mashamba ya John Waller, akagundua kuwa mama yake alishauzwa katika mashamba mengine na kwamba baba yake tayari alishafariki kwa kuvunjika moyo miaka miwili iliyopita.

 

Mwaka 1822 akalipata kaburi la baba yake baada ya kulitafuta kwa muda mrefu, akaliwekea msalaba wenye jina la Toby ,jina lake la kitumwa badala ya Kunta Kinte, kizzy pia ni mmoja wa wahenga wa mwandishi huyu, Haley, ambaye ana vinasaba sawa na Kunta Kinte ,aliyetumia maisha yake yote utumwani.

 

Sehemu ya mbele nyingine katika kitabu, inaelezea kizazi kati ya Kizzy na Alex Haley walielezea matatizo waliyoyapata, hasara na ushindi mkubwa walioupata huko Marekani, Alex Haley alidai kwamba yeye ni kizazi cha saba kilichomfuatia Kunta Kinte. Haley alidai kwamba vyanzo asilia kabisa vya simulizi ya Kunta Kinte kaitoa kwa familia asilia ya Gambia na mtu aliyempatia ni wa huko Gambia aitwaye, Kebba Kanga Fofana, aliyedai kuwa alikuwa ni msimuliaji aliyekuwa na taarifa juu ya ukoo wa Kunta Kinte.

 

Aliielezea familia ya Kunta Kinte kuwa, wanaume walikuwa wakijihusisha na shughuli za uhunzi, wakitokea katika jamii ya kiislamu, ,Kairaba, Kunta Kinte asili yao ni huko Mauritania, Haley alimnukuu Fofana kwamba alimweleza kuwa ” Wakati huo kati ya Vijana hao wanne ,Kunta ,aliondoka kijijni hapo kwenda kukata kuni na ndipo akapotea bila kuonekana tena.”

 

Ingawa baadae waandishi wa habari na wanahistoria waligundua kwamba Fofana hakuwa msimuliaji wa jamii ya Gambia.Mara aliposimulia kwa mara ya pili simulizi ya Kunta Kinte, Fofana alibadilisha baadhi ya sehemu muhimu, ikiwemo ile ya jina la Baba yake, majina ya kaka na Dada zake, umri wake, na hata mwaka ambao alipotea ,pia katika sehemu mojawapo alisema kwamba, Kunta Kinte alikuwa katika kizazi ambacho kilikuwa hai hadi karne ya 20, pia ikagundulika kwamba wazee na wasimuliaji hawakuweza kutoa habari za mtiririko wa familia Kabla ya katikati mwa karne ya 19.

 

Baada ya kitabu cha Haley “Roots” kuwa maarufu kitaifa nchini Amerika ,mwandishi wa Amerika, Harold Courlander, Alisema kwamba Sehemu ya Kitabu hicho cha Roots inayoelezea kuhusu maisha ya Kinte ilichukuliwa kutoka katika Riwaya ya Courlander iitwayo”The African” mwanzoni Haley alikataa katakata tuhuma hizo, lakini baadae akatoa taarifa kwa umma akithibitisha kwamba kitabu cha Courlander ndicho alikopata simulizi za Kunta Kinte .

 

Courlander akamshtaki Haley kwa wizi wa hakimiliki jambo ambalo Haley alitaka wamalizane nje ya Mahakama, na ikawa hivyo. Kunta Kinte limekuja kuwa jina maarufu sana duniani, ni sawa na jina la wafuasi wa kibwetere lililokuwa linatajwa katika nyanja mbalimbali wakiwemo wasanii wa bongofleva nchini Tanzania.

 

Vilevile jina Kunta Kinte limetumika sehemu mbalimbali kwa wasanii nk.

Kwenye ile tamthilia ya “Fresh Prince of Bel–Air”, mhusika wa Will Smith, anasema ” kwanini sasa usinifanye kama Kunta Kinte na kunikata mguu wangu? “.

 

Repa na mtunzi wa nyimbo, Kendrick Lamar,alimtaja Kunta Kinte mwaka 2015 kwenye singo yake ” king Kunta ”

Naye busta rhyme Katika nyimbo yake ya “rhymes galore” 1997 kamtaja Kunta.

Missy Elliott kwenye “work it” pia Ludacris katika nyimbo ” coming 2 Amerika ” kamtaja Kunta Kinte katika albamu yake ya “Word of Mouf”
Kwenye Barbershop eneo la kuchezea filamu ya “Coming to America ” myahudi alimuita Akeem “Kunta Kinte”.


Toa comment