The House of Favourite Newspapers

Kupinga Madawa Ya Kulevya… Dar Live Kukusanya Jogging Clubs 20

Jogging

Na Mwandidhi wetu | RISASI JUMAMOSI | MIKITO NUSUNUSU

UWANJA wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar unatarajiwa kukusanya zaidi ya klabu 30 za Jogging Machi 12 (kesho), mwaka huu katika bonanza maalum la kupinga matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo (pichani) alisema kuwa kauli mbiu ya vita hivyo ni Kijana Acha Madawa, Kamata Fursa Jiongeze Kimaisha.

“Listi ya klabu hizo ni ndefu sana lakini naweza kutaja vilabu vichache ambavyo ni Dar Jogging, Temeke Family Jogging, Biafra Jogging, Majenga Group Jogging, Kiburugwa Jogging, Wasafi  Jogging, Kopa Jogging, Mzimuni Jogging, Goms Jogging, Wakali Jogging, Tandale Kwanza Jogging, Ukonga Jogging, Magenge 20 Jogging, Yombo Family Jogging na vingine vingi,” alisema Mbizo.

Comments are closed.