The House of Favourite Newspapers

Kusah: Aunt Ndiye Amenifanya Hivi Nilivyo

0

KATIKA safari ya mafanikio ya maisha ya binadamu, kila siku lazima uvuke milima na mabonde ili ufike kwenye ngazi ya mafanikio.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wengi maarufu na wenye majina makubwa. Hawa wana historia ya kuumiza, kujifunza na hata kufurahisha kwa wakati mwingine.

 

Hicho ndicho alichopitia msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Salmini Hoza almaarufu Kusah. Kabla ya kuwa staa anayesikilizwa zaidi kupitia ngoma yake ya I Wish huko nyuma alifanya kazi mbalimbali ili kumuingizia kipato cha kila siku huku akiwa hatarajii kabisa kama ipo siku atafahamika na watu mbalimbali. Hakufikiria kama kuna siku atamiliki mtoto mzuri kutoka tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel na kubarikiwa mtoto mmoja wa kiume, Nono.

 

Gazeti la IJUMAA limekaa kitako na Kusah kwenye mahojiano maalum (exclusive interview) ambaye anaeleza wazi msoto alioupitia huko nyuma mpaka alipofika hivi sasa;

IJUMAA: Vipi Kusah, habari ya wewe?

 

KUSAH: Salama kabisa, vipi hali, natumaini leo mambo yatakwenda sawia?

IJUMAA: Vipi kuhusu mapokeo ya I wish?

KUSAH: Kwa kweli mapokeo ni makubwa mno, kinyume kabisa nilivyotarajia kuanzia kwenye kuirekodi na kila kitu.

 

IJUMAA: Kwa nini umesema hivyo?

KUSAH: Yaani kwa sababu hata siku nairekodi ilikuwa ni siku ya birthday ya Mama Nono, walikuwepo mastaa kibao pale hivyo nilivyoirekodi, huwezi amini ilipokelewa vizuri sana na baada ya hapo ikafungua milango ya mafanikio yangu kitu ambacho sikikutarajia kabisa; maana hata watu ambao walinichukulia poa, sasa wananiheshimu.

 

IJUMAA: Kumbe kuna watu walikuwa wakikuchukulia poa?

KUSAH: Wengi sana, kuna wakati hata unamuomba mtu akupostie wimbo wako hataki tu na wala hakupi sababu, lakini hivi sasa mtu anaposti mwenyewe bila hata kumwambia ndipo hapo naamini kabisa wakati wa Mungu ndiyo wakati sahihi siku zote.

 

IJUMAA: Kuna changamoto zozote ulikutana nazo huko nyuma?

KUSAH: Ni nyingi sana mpaka nafika hapa nilipo. Hii ni kwa sababu kazi ni nyingi sana. Nakumbuka nilikuwa bodaboda na nilishakuwa kinyozi mzuri tu kipindi hicho nilikuwa nyumbani kwetu Bumbuli (Tanga), lakini nilikuwa nafanya yote hayo nikiwa ninaimbaimba na kupiga vishoo vya bure; yaani ni kitu ambacho kilikuwa kwenye damu.

 

IJUMAA: Ilikuwaje hadi sasa ukatoboa mpaka ukafika huku?

KUSAH: Ni kwenye kutafuta maisha maana niliondoka Tanga kuja huku Dar, baba yangu alikuwa akiishi huku na hapohapo nikaanza kujiongeza mwenyewe kwa kujipenyeza huku na huku ingawaje haikuwa rahisi, maana ilikuwa ninaenda hata kutafuta shoo za bure niimbe bila hata kulipwa na bado hawakutaka kabisa, hapo sasa kama una roho ngumu unaacha kila kitu.

 

IJUMAA: Ilikuwaje sasa ukakutana kwanza na Ruby?

KUSAH: Ni katika mambo ya muziki hayohayo na hapo ndipo nilipoanza kujulikana kidogo ingawaje na watu bado walikuwa hawajakubali vizuri muziki wangu mpaka nilivyojitahidi sana.

IJUMAA: Ulivyokutana na Aunt mambo yalibadilika?

 

KUSAH: Sana na siwezi kueleza Aunt ndiye amenifanya mimi kuwa hivi nilivyo leo, amenipa mtoto mzuri, ananiheshimu kama mumewe na amefanya pia watu wengine kuniheshimu sana.

IJUMAA: Mara nyingi kwenye video zako kama mbili unapenda kumtumia Aunt kama video queen, je, ni kwa nini?

KUSAH: Kwanza ni mzuri na anastahili, kwa nini nipate shida na wakati nina chombo ndani?

 

IJUMAA: Vipi wivu, maana Aunt ni mwanamke mrembo sana na ni staa anayejulikana na watu mbalimbali?

KUSAH: Wivu upo mwingi sana kwa mke wangu, mno na kwa sababu tu nampenda, kuna wakati natamani asitoke hata ndani kabisa, lakini mwisho wa siku lazima atoke na kuhangaika na yeye kama ilivyo kwa watu wengine.

 

IJUMAA: Umeachia wimbo mwingine wa I Don’t Care hivi karibuni, vipi mapokeo yake?

KUSAH: Namshukuru sana Mungu, umepokelewa vizuri sana kwa kweli.

IJUMAA: Haya nakushukuru sana Kusah.

KUSAH: Asante sana.

 

MARA nyingi kwenye video zako kama mbili unapenda kumtumia Aunt kama video queen, je, ni kwa nini?

KUSAH: Kwanza ni mzuri na anastahili, kwa nini nipate shida na…

Makala; Imelda Mtema, Bongo

Leave A Reply