Kushuka kwa kizazi ( Prolapsed uterus)

Kushuka-kwa-kizazi--(-ProlaKizazi kimeshikiliwa vizuri sehemu yake kwenye nyonga na misuli, tishu na nyuzinyuzi ngumu ziitwazo ‘ligaments’ ambazo zimejishika kwenye mifupa ya nyonga kwa ujumla ili kuleta uimara.

Viungo hivi vinaweza kupoteza uimara wake na kuwa dhaifu kutokana na uzazi au uzazi kuwa na shida. Tatizo hili pia linaweza kuwapata wanawake watu wazima waliofikia ukomo wa kuzaa au ambao kiwango cha vichocheo vya ‘estrogen’ vimepungua mwilini hasa anapofikia ukomo wa hedhi.

Tunaposema kizazi kimeshuka, ina maana kizazi kipo katika njia ya uke ‘vaginal canal’. Kwa hiyo kizazi kinaweza kushuka kidogo au kikashuka chote na kigusa kabisa ukeni kwa nje.

HATUA ZA KUSHUKA KIZAZI

Zipo hatua nne za kushuka kizazi ambapo sasa tunasema kizazi kimeshuka.

Hatua ya kwanza; ‘first degree’ mlango wa kizazi badala ya kuwa juu unakuwa ukeni. Hapa mwanamke wakati wa kujisafisha atahisi kitu kama golori ukeni kwa ndani kidogo. Pia atahisi maumivu wakati wa tendo la ndoa kama kuna kitu kinasukumwa.

Hatua ya pili; mdomo wa kizazi unapatikana katikati ya uke. Hapa ukiingiza vidole ukeni unahisi mdomo wa kizazi upo jirani katika mlango wa uke.

Hatua ya tatu; mdomo wa kizazi unajitokeza kwa nje ya uke, hatua hii hata ufanyaji wa tendo la ndoa unakuwa mgumu.

Hatua ya nne; kizazi kinakuwa nje kabisa ukeni na kinaning’inia kwa nje. Hali ikishafikia hapa kitaalam tunaita ‘Procidentia’. Hapa inaashiria udhaifu mkubwa katika viungo vyote vinavyoshikilia kizazi kama tulivyoona hapo awali.

Pamoja na kwamba tatizo hili hutokea kwa wanawake watu wazima na wazee, hatua ya kwanza kama tulivyoona huwatokea hata wasichana au wanawake walio katika umri wa kati kutokana na matatizo mbalimbali kama uwepo wa maambukizi sugu ya kizazi na mlango wa kizazi, uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi hasa ‘Fibroid’ na matatizo mengine ya mfumo wa homoni yanayosababisha homoni ya ‘Estrogen’ kupungua. Kupungua kwa homoni ya ‘Estrogen’ kunaweza tu kutokea kwa bahati mbaya au kutokana na matumizi ya muda mrefu ya dawa za homoni bila ya mpangilio maalum.

Matatizo mengine yanayosababisha hali hii ni kama vile.

Itaendelea wiki ijayo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS
GLOBALBREAKINGNEWS.JPG


Loading...

Toa comment