KUSINIGHT: MASTAA 12 KUMSINDIKIZA HARMONIZE IDD DAR LIVE LEO

Harmonize

MASTAA 12 akiwemo Ben Pol, Nyandu Toz, Dulla Makabila, Rommy Jones, Huddah ‘The Boss Chick’ Chin Bees pamoja na Queen Darleen wanatarajiwa kumsindikiza staa mwenzao kunako Muziki wa Bongo Fleva, Harmonize katika shoo ya Sikukuu ya Idd Pili, leo Jumamosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, Idd Pili shoo nzima itaanza mapema kuanzia saa 12 za jioni ambapo itakuwa bandika bandua kutoka kwa wakali hao huku Madj wanne wakisimamia shoo nzima ambao ni DJ Seven, DJ Cavan, RJ The DJ ‘Rommy Jones’ pamoja na RDJ Mammie.

 

“Mtangazaji wa shoo nzima ni mwanadada kutoka Kenya, Huddah the Chick Boss ambaye amepania kwelikweli kuiendesha shoo nzima mwanzo mwisho.

“Najua mashabiki wengi watakuwa wakisubiri kwa hamu kushuhudia Harmonize akipafomu Kwa Ngwaru lakini pia watambue timu nzima ya WCB itahamia Dar Live kuanzia madansa hadi wanamuziki,” alisema KP.

 

NGOMA ZA HARMONIZE HIZI HAPA

Miongoni mwa ngoma zitakazotikisa Idd Pili hii ni Happy Birthday, Bado, Matatizo, Shulala, Nishachoka, Kidonda Changu, Penzi, Sina, Acha Nilewe, Niambie, Aiyola na nyingine kibao.

MTONYO SASA

Shoo nzima itakwenda kwa kiingilio cha shilingi elfu 10, tu getini. Jitahidi kuwahi usije ukapata siti za nyum

Mikito Nusunusu.

 

Msikie Harmonize Akifungukia Shoo ya Kusi Night, Dar Live


Loading...

Toa comment