The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Kutana na Mchungaji Zimbabwe ‘Anayeongea na Mungu kwa Simu’ Madhabahuni

0

MAAJABU!  Mchungaji nchini Zimbabwe, Paul Sanyangore wa Kanisa la Victory World International amewashangaza waumini wake kanisani alivyopiga simu na kusema kwamba alikuwa anaongea  na Mungu.

Mchungaji huyo alifanya hivyo mbele ya kadamnasi ya waumini wake kwa kupiga namba ya simu ya Mungu na kuanza kuongea naye akizunguka kanisani hapo ambapo waumini wake walikuwa wakimpigia makofi na vigelegele.

Sanyangore alifanya hivyo wakati anamuombea mwanamke mmoja aliyekuwa anataka msaada kwake kutokana na wanaye wawili wenye matatizo ya kifafa na pumu.

Kiongozi huyo ‘mtata’ wa dini aliwahi ‘kuibariki’ mipira ya kiume (condom) kwa ajili ya kutumiwa na waumini wake.   Isitoshe hivi majuzi alisema kwamba atawapa waumini wake namba ya simu ya Mungu ili waweze kumpigia wanapotaka.

Leave A Reply