The House of Favourite Newspapers
gunners X

KUTEKWA MO, LEMA AHOJIWA POLISI SAA 3, ATOA ‘POVU’ ZITO – VIDEO

MBUNGE wa Arusha Mjini (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema leo Oktoba 12, 2018, amehojiwa na Kamanda Mkuu wa Polisi mkoani humo katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa takribani saa tatu juu ya anachokifahamu kuhusu tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji  wa jijini Dar es Salaam.

Lema ambaye jana alipigiwa simu na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi,  na kumtaka afike kituoni hapo leo, amewasili akiwa ameongozana na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure.

 

“Jana nilipokea simu kutoka kwa viongozi wa polisi wakinitaka nifike jana usiku, lakini nilikuwa mbali hivyo nikaomba nifike leo, hawakuniambia wananiitia nini lakini nilihisi ni mambo ya press yangu niliyozungumza Dar kuhusu kutekwa kwa Mohammed Dewji.

 

“Nimeandika kile ambacho nakijua na ni kile nilichokizungumza kwenye press, nimesema sitoacha kulikemea jeshi hilo na kulionya pale nitakapoona panafaa kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani. Kuna mashaka ambayo wanayo watu wengi kuhusu yaliyojitokeza kwenye hili suala, huwezi kuondoa mashaka hayo kwa kutisha watu bali kwa kuleta majibu, hivyo wasiyapuuze.

 

“Nipo tayari popote na kwa yeyote ku-defend kile nilichokisema kuhusu utekaji. Wakisoma wataona hiyo wanayosema kuisaidia polisi na nimewasaidia kwelikweli, hivyo,” alisema Lema.

 

Akizungumzia kuhusu Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuzuia wananchi wasifanye mijadala ya tukio la utekani, Lema amesema waziri huyo hawezi kuzuia wananchi kuzungumza.

 

“Nimemwambia RPC wakinihitaji hakuna haja ya kufanya sinema za zamani za kuruka ukuta na kukata fensi, wanipigie tu nitakwenda mwenyewe kwa nauli yangu wala sitatumia mafuta yao,” alimaliza lema.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lema ameandika: Polisi wameniuliza maswali juu ya utekwaji wa Mo. Nimesema kuwa kutekwa kwa Mo na kupatikana kwake kumeacha wasiwasi mwingi. Naamini kama Biblia ingekuwa bado inaandikwa pengine suala hili lingeandikwa kama muujiza,” amesema Lema.

Masaa 3 Lema Kuhojiwa POLISI Kuhusu MO Atoka na Kutema cheche

Comments are closed.