The House of Favourite Newspapers

Kutoka Kahama… Wanasiasa Washtukiwa

0

IMG_0786 Mji wa Kahama

KAHAMA: Umoja wa wafanyabiashara katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wamewashtukia wanasiasa kwa tabia yao ya kupoka miradi ya wawekezaji na kudai wameitekeleza wenyewe.

IMG_20160503_125728Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama (Picha na Maktaba).

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Wilaya ya Kahama, Shilinde Samandito alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Halmashauri kilichowajumuisha wao, taasisi za umma, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abel Shija.

IMG_0789

Aliwataka wawekezaji waliopo wilayani hapo, ukiwemo mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia kuweka wazi shughuli zao kwa jamii ili kuepusha udanganyifu unaofanywa na wanasiasa kwamba shughuli hizo zinatekelezwa na wao.

Hilo lilijiri baada ya Mwenyekiti wa Halmashauri, Shija kutamka kuwa mtambo wa kusambaza umeme katika mji huo uliotolewa na mgodi wa Buzwagi upo katika hatua ya mwisho, kitu kilichowashangaza kwani kwa muda mrefu, wanasiasa wamekuwa wakijitapa kuwa ndiyo watekelezaji wa mradi huo.

“Sisi kama Wafanyabiashara kwa hili mnalotueleza kuwa mgodi wa Buzwagi upo hatua ya mwisho katika zoezi la ukamilishaji wa mtambo wa kusambaza umeme wa uhakika mjini Kahama, mnatupa wakati mgumu, tumuelewe nani kati yenu wanasiasa ama ninyi? Wanasiasa wanajinadi kuwa mtambo huo wanauleta wao, ” alisema Samandito.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo, Vita Kawawa akizungumza katika kikao hicho, aliutetea mgodi huo na kudai umetekeleza miradi mingi ikiwamo barabara za Kahama mjini zenye urefu wa kilometa tano, zahanati ya kisasa katika Kata ya Mwendakulima, ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwendakulima na sasa wana mpango wa kuweka taa za kuongozea magari.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Mji na Miundombinu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Benard Mahongo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Majengo alisema wameamua kuwaalika wafanyabiashara wa mji huo, taasisi za umma pamoja na viongozi hao wa kisiasa ili waone miradi inayotekelezwa na halmashauri hiyo kuepuka tafsiri potofu kutokana na kupata taarifa zisizo rasmi mitaani.

Leave A Reply