KUTOKA MANCHESTER: Hali Ilivyo Kuelekea Mchezo Dhidi ya BARCA!
Mashabiki wa Machester United wameonesha kuwa na hali ya kujiamini kuelekea mchezo wa robo fainali wa vilabu bingwa Ulaya dhidi ya mabingwa FC Barcelona kutoka nchini Hispania.
United wanavaana na Barca kwenye Mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo mechi itakayochezwa Uwanja wa Old Traford jijini Manchester.
Global TV Online, Gazeti la Championi na Spoti Xtra wamefunga safari mpaka jiji la Manchester na kufanikiwa kupata nafasi ya kuingia kwenye uwanja wa Old Trafford kushuhudia game hiyo, na watakuletea matukio yote yatakayojiri huko, endelea kuwa nasi.


Comments are closed.