The House of Favourite Newspapers

Mwanza: Wauawa kwa Kuwatapeli Wafanyabiashara

0

kamugishaKamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Justus Kamugisha.

Stori: Mashaka Baltazar, RisasI Jumamosi

Watu wawili wakazi wa Maswa Mkoani Simiyu, wameuawa na wananchi wenye hasira kali katika Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakituhumiwa kuwatapeli fedha wafanyabiashara wa mifugo.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni saa 7:00 mchana katika mnada wa mifugo uliopo katika Kijiji cha Maligisu Tarafa ya Ibindo.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Agustino Senga aliwataja waliouawa kwenye tukio hilo kuwa ni Daud Joseph (32) na Mzee Magashi (40) wakazi wa Stendi Mpya ya wilayani Maswa.

Alisema kuwa, Joseph alishambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa fimbo na mawe hadi kufariki dunia papohapo kisha wakamkimbiza mwenzake Magashi hadi katika Kijiji cha Jija, walipomkamata walimshambulia kwa mawe na fimbo hadi kufa.

Senga alieleza kuwa marehemu hao walikuwa wakituhumiwa kuwa na tabia ya kuwatapeli wafanyabiashara wa mifugo kuwa watawauzia ng’ombe na kupewa fedha kisha kuingia mitini.

Hata hivyo, siku ya tukio watuhumiwa hao ambao tayari walikuwa wamewaliza wafanyabiashara wengi walionekana mnadani hapo ndipo wakapigiwa kelele za ‘weziiiii’ na kukiona cha mtemakuni.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply