The House of Favourite Newspapers

KWA HAYA MONDI , KIBA MUAMKE TU

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,

UNAKUM-BUKA vile vibweka vya mwenye kiti chake amerudi? Ally Salehe Kiba aliyekuwa amepotea kwenye gemu takriban kama miaka mitatu hivi, alirejea na kukuta muziki umeshikiliwa na bwana’ mdogo kutoka Tandale, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akasema mwenye kiti chake amerudi.  Kiba aliitoa kauli hiyo akiwa ana maana kwamba, yeye ndio mwenye muziki wake. Akawaaminisha Watanzania kwamba sasa anarudi kuchukua namba moja yake ambayo alikuwa ameiacha na Diamond akawa ameshika kwa muda. Akafyatua ngoma mbili za harakaharaka, Mwana na Chekecha Cheketua anga la burudani likachafuka. Kwa vyovyote vile upepo ule ulimsumbua Diamond. Mnyukano ukawa mkali sana mitandaoni.

Katika mnyukano huo, iliibuka hoja kubwa iliyokuwa inambeba Kiba kwamba jamaa anaujua muziki. Diamond naye alibebwa na hoja ya kwamba anaijua biashara ya muziki. Waliomtetea Kiba walijivunia kwamba ni mwanamuziki ambaye muziki wake unajiuza kuliko Diamond atatumia nguvu nyingi sana kumpoteza Kiba.

Waliokuwa wanamtetea Diamond hawakuwa na hoja sana ya kushikilia maana walizidiwa hoja ya uanamuziki maana kweli Kiba alikuwa fundi wa muziki. Kiba alikuwa na sauti fulani hivi ya kipekee ambayo ilikuwa inampa ushindi hata kabla hawajashindanishwa. Kiba alibebwa na ukongwe. Alikuwa Mfalme wa Bongo Fleva kiasi cha Mwanamuziki wa Marekani, R Kelly kumchukua na kufanya naye kolabo ya kimataifa iliyokwenda kwa jina la Hands Across The World kupitia project iliyoitwa One 8.Related image

Mijadala ya kulinganisha nyimbo zao ikatawala kila kona na kila walipokuwa wakitoa ngoma, mashabiki walikuwa wakifuatilia ipi imepata wafuasi wengi kuliko nyingine. Unakumbuka Diamond alishirikishwa na Fid Q Wimbo wa Fresh Remix akamchana sana Kiba naye akamjibu kwa Wimbo wa Aje. Hoja nyingine iliyoibuliwa na wafuasi wa Kiba ilikuwa ni kwamba, msanii wao ametangulia kuliona jua. Kiba ni mkubwa kuliko Diamond. Kiba ameanza muziki wakati Diamond bado hata hajafikiria kuwa mwanamuziki.

Hoja hiyo ndiyo iliyompa hasira sana Diamond kuhakikisha anapambana na kaka yake kimuziki. Alijua uwezo wa Kiba hivyo ili kuwa mkubwa, alihitaji nguvu ya ziada kutokana na kuwa mwenzake alikuwa na mashabiki wengi waliommisi, ilikuwa rahisi sana kumzidi. Mnyukano wa kimuziki ulihama kutoka kwenye mambo ya kimuziki, watu wakahamishia vita katika masuala yao ya kimafanikio. Wakawa wanafuatilia jinsi wasanii hao wanavyoj-idhatiti katika masuala ya maendeleo.

Diamond akakamilisha mjengo kule Madale, Kiba naye akasema isiwe kesi. Akajipinda mpaka na yeye akakamilisha mjengo wake kule Tabata. Diamond akaanzisha Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB), Kiba naye hakuwa nyuma, kupitia Rockstar4000 ambayo yeye ni moja ya wakurugenzi, wamewasainisha baadhi ya wasanii katikia lebo hiyo akiwemo Ommy Dimpoz.

Diamond akachukua nyumba nzima maeneo ya Mapambano Sinza jijini Dar, akaifanya ndiyo ofisi ya Wasafi ambayo ilikuwa na vichwa vikali kama Harmonize, Rayvanny, Lava Lava na Mbosso ambao wote kwa sasa wanajiuza, wanapiga mkwanja kupitia kampuni hiyo.

Kwenye eneo hilo Diamond akaanza kumpiga gepu taratibu Kiba. Haikupita muda mrefu sana, Diamond akashusha bonge la mjengo lingine ambalo hilo alilitumia kushusha studio zake za Wasafi TV. Kwenye TV hiyo, Diamond akaajiri vijana kibao.

Kuhusu shoo, Diamond ameonekana kumkimbiza sana Kiba kwani mara kibao amekuwa akifanya shoo za nje ya nchi huku Kiba akijitutumua mara chache sana. Diamond na familia yake, ni mabalozi wa supermarket, ni balozi wa Kampuni ya simu, usisahau kuhusu Diamond Karanga na Chibu Pafyumu, kwenye tuzo za muziki ndiyo usiguse kabisa.

Kiba alikuja na kinywaji, hakijulikani kimeishia wapi kwani mpaka sasa bado hakijaingia mtaani. Kolabo za kimataifa, Diamond amefanya nyingi pande za Nigeria ukiwemo Wimbo wa Number One Remix aliofanya na Davido, Fire aliofanya na Tiwa Savage, Halleluja aliofanya na Morgan Heritage wa Jamaica.

Kuna Nana aliyofanya na Mnigeria Mr Flavor, kuna Kidogo aliofanya na P-Square. Kuna African Beauty aliofanya na Omarion wa Marekani, Waka Waka aliyofanya na Rick Ross, Marry You aliyofanya na Neyo. Usisahau hapo Sauz, amefanya na A.K.A ngoma inaitwa Make Me Sing, Chacun Pour Soi aliyofanya na Papa Wemba kutoka Kongo. Kwa upande wake Kiba, anajivunia kolabo yake na Jude Abaga ‘M.I’ wa Nigeria ambaye amefanya naye Aje Remix, halafu ana Unconditionally Bae aliyofanya na Kundi la Sauti Sol la Kenya.

Kwa upande mwingine, Diamond anavitega uchumi vya viwanja, ana nyumba Tandale, ana nyumba Sauz jambo ambalo linahitaji nguvu ya ziada kwa Kiba kumfikia. Ukiweka kwenye mizani mafa-nikio aliyonayo Diamond na Kiba, utagu-ndua licha ya kuwa Diamond ni mdogo kiumri lakini kimafanikio ya muziki na maisha, Kiba anapaswa kumheshimu Diamond!

Comments are closed.