The House of Favourite Newspapers

Kwa JKT Queens Ukinuna Uwe na sababu

Wachezaji wa timu ya JKT Queens.

JKT Queens imeweka rekodi ya kipekee kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Women’s Premier League baada ya kucheza michezo 11 ya mzunguko wa kwanza sawa na dakika 990 kwa kufungwa mabao matatu pekee.

 

Mabingwa hao watetezi wamekuwa na safu kali ya ushambuliaji ndani ya ligi ya wanawake kwani katika michezo hiyo 11 wamefunga mabao 72 sawa na wastani wa kushinda mabao zaidi ya matano katika kila mechi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha wa JKT Queens, Ally Ally alisema; “Sisi ni mabingwa watetezi tuna kazi ya kuendelea kuifanya kwa hali na mali kuona tunafi kia lengo la kubaki na kombe letu kama ambavyo
tulifanya msimu uliopita, ushindani ni mkubwa ila sisi tuna uzoefu na juhudi.”

 

Wakati JKT Queens wakiwa ni vinara wa Ligi ya Wanawake baada ya kufi kisha pointi 33, Mapinduzi Queens inaburuza mkia ikiwa na pointi mbili baada ya kucheza michezo 11.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

Comments are closed.