The House of Favourite Newspapers

Kwa Mara ya Kwanza, Dayna Nyange Anyakua Tuzo za Kimataifa

MWANADADA matata kwenye game ya Bongo Fleva, Dayna Nyange amekuwa Mtanzania pekee kuibuka mshindi wa Tuzo mbili za BAE Awards 2017zilizofanyika nchini Nigeria.

Dayna Nyange ameshibnda vipengele viwili ambavyo ni BEST AFRICAN ACT alichokuwa akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana) pamoja na Jah Vinci (Jamaica).

Pia ameshinda Kipengele cha BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo alikuwa akiwania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria).

Ni kwa mara ya kwanza masanii huyo kuchaguliwa na kushinda  tuzo za Kiamataifa baada ya kupata nafasi kwenye tuzo hizo nchini Nigeria.

Akizungumza na Global Publishers kuelezea furaha yake baada ya kunyakua tuzo hizo Nyange amesema;

“Leo imekuwa siku yangu ya furaha sana sana sana, ningependa ni washukuru wotee mliokesha mkiniombea, mlikesha mkihamasisha, mlikesha mkinipigia kura. Hatimaye tumefanikiwa kutwaa tuzo zote mbili nchini Nigeria.

BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE

BEST AFRICAN ARTISTE

Nawashukuru sana mashabiki zangu, ahsanteni sana wadau wangu, ahsanteni sana Media zote, watangazaji, waandishi, na Ma Dj. Pia Namshukuru producer wangu Mr. Ttouch, shukrani kwa menejiment yangu na wasanii wenzangu.

Sote tuliacha kazi na tukafanya kazi moja tu na hatimaye matunda ni haya. Sijashinda mimi tu @daynanyange bali imeshibda Tanzania na Afrika kwa ujumla. JuhudiZimezaaMatunda. Mungu awabariki sana.” Alisema Dayna Nyange.

Imeandikwa na Edwin Lindege

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.