The House of Favourite Newspapers

Kwa Mara ya Kwanza, Madaktari Wafanikiwa Kupandikiza Uume

JOPO la madaktari wamefanikiwa kufanya upandikizaji wa kwanza wa uume na korodani ambapo askari alijeruhiwa na bomu huko Afghanistan amefantiwa tiba hiyo katika Chuo cha Johns Hopkins mjini Baltimore, Maryland,

Madaktari hao walitumia uume na korodani zilizoondolewa kwa watu waliokufa (maiti). Madaktari hao wamesema askari huyo atarudishiwa uwezo wa kufanya mapenzi, jambo ambalo sio rahisi kama mtu akifanyiwa upasuaji wa uume.

Upasuaji huo uliofanyika machi 26 mwaka huu, ulifanyika mara 11 na upandikizi ukitumia saa 14, huku ukiwa ni upasuaji wa kwanza kumalizika salama na kurejesha sehemu hizo katika hali yake ya kawaida. Madaktari wanasema kwamba korodani kutoka kwa mfadhili hazijapandikizwa kutokana na sababu za maadili.

 

Askari aliyefanyiwa upandikizaji ametaka kutofahamika “Nilipoamka nilijisikia kuwa nimerudi kwenye hali yangu ya kawaida, kiukweli niko sawa kwa sasa,” alisema askari huyo. Wataalamu wa upasuaji huo wanatarajia kuwa askari huyo atapona ndani ya miezi 6 hadi 12.

Comments are closed.