The House of Favourite Newspapers

Kwa mara ya kwanza Tiffah live!

0

TIFFAH DIAMOND (4)Staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenzake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakimtoa mtoto wao, Latiffah Nasibu ‘Princes Tiffah’.

  • Sherehe yake ya 40 usipime, Zari, Diamond waandika historia

Na waandishi wetu

YAMETIMIA! Baada ya kutoonekana sura kwa zaidi ya siku 40 tangu azaliwe, hatimaye mtoto wa mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifah ‘Tiffah’ ameonekana hadharani (live), Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kuripoti.

TIFFAH DIAMOND (5)Diamond na Tiffah

Tukio hilo la kihistoria kwa Diamond na mzazi mwenzake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ lilichukua nafasi jana, nyumbani kwake Madale-Tegeta jijini Dar.

Waandishi wetu, Musa Mateja na Imelda Mtema waliokuwepo kwenye tukio hilo mwanzo-mwisho waliripoti live Makao Makuu ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge:

Saa 7 mchana

MAANDALIZI

Makao Makuu: Mateja na Imelda mbona kimya nini kinaendelea huko?

Imelda: Mkuu huku mambo ndiyo yameiva, maandalizi ni bab’kubwa, pamepambwa pakapambika kila sehemu. Ongea na Musa huyu hapa…

Musa Mateja: Hapa nawaona watoto  wa ‘kaswida’ wakianza kwa utangulizi wa nyimbo za kumtukuza Mungu. Mkuu…Mkuu…ngoja nikuunganishe na Imelda naona ana kitu anataka kukujuza…

Saa 7.15 mchana

MPOTO AWA KIVUTIO

Imelda: Dah! Namuona msanii Mrisho Mpoto akicheza kaswida kwa ufundi mzuri na kuwa kivutio kwa waalikwa huku wengine wakishika midomo yao.

Makao Makuu: Wasanii gani wengine walioonekana?

Imelda: Naiona Timu Kajala Masanja (muigizaji) ikiingia eneo la tukio, huku Kajala akiwa mbele akifuatiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi, Halima Kimwana (dada wa hiari wa Diamond) na muongoza sinema, Leah Mwendamseke ‘Lamata’.

Saa 8:00 mchana

MABAUNSA 11 WASIMAMIA ULINZI

Makao Makuu: Imelda vipi kuhusu ishu ya ulinzi?

Imelda: Ulinzi toka asubuhi upo wa kutosha, kila kona kuna baunsa. Mabaunsa 11 wamejigawa kila kona kuhakikisha usalama.

Saa 9:00 alasiri

ZARI APAMBWA

Makao Makuu: Mbona kimya tena kunani?

Imelda: Ama kweli ustaa noma! Namuona Zari anapambwa na wapambaji kama 6 hivi, akijiandaa kutoka rasmi, itakuwa mtoto anataka kutolewa sasa Mkuu.

SEHEMU YA KUKAA MOTO

Makao Makuu: Mateja vipi kuhusu eneo atakalokaa Zari na mwanaye?

Mateja: Mkuu mtoto aliandaliwa sehemu maalum ya kukaa akiwa kabebwa na mama yake na sehemu hiyo viti vimetawaliwa na rangi ya dhahabu na rangi nyeupe.

MABAUNSA KAMA FBI

Mateja: Mabaunsa wote wamevaa suruali nyeusi, T. Shirt na makoti meusi kama vile wavaavyo Shirika la Kipelelezi la Kimarekani (FBI).

TIFFAH KAMA DIAMOND

Imelda: Mkuu sasa Tiffah ndiyo ametolewa nje. Kwa wale waliokuwa na walakini kuhusu mtoto huyo kufanana na baba yake watakuwa wameupata ukweli, hapa kila mtu anasema Tiffah ni Diamond mtupu!

Saa 10:00 jioni

ZARI, DIAMOND WAFUNIKA

Mateja: Baadhi ya wahudhuriaji wa sherehe hii waliozungumza na Ijumaa Wikienda, wamesema Zari na Diamond wamefunika kwani sherehe za aina hii zimeshafanywa na mastaa wengi lakini hii ni funika bovu.

“Diamond na Zari hakika wamefunika. Wameandika historia. Tumeona sherehe nyingi za aina hii lakini hii ni kiboko yao. Kuanzia ulinzi, kadi maalum za mwaliko, mapambo, vyakula, vinywaji hakika ni gharama kubwa sana kuliko sherehe nyingi za mastaa tulizowahi kuzishuhudia hususan hizi za kutoa watoto,” alisema mmoja wa wahudhuriaji ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.

Makao Makuu: Basi sawa endeleeni kupiga kazi, picha zingine ambazo tutakuwa hatujazipata mtakabidhi ofisini Jumatatu (leo) asubuhi.

Leave A Reply