Kwa Mara Ya Kwanza Tuzo za Trace 2025 Kufanyika Zanzibar – Video
Tuzo za Trace Music Awards zinatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar, Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar leo, mmoja kati ya wadau wa tuzo hizo, Christina Mosha ‘Seven’, amesema kuwa katika tuzo hizo wasanii wa Bongo Fleva nchini watapata nafasi ya kushiriki tuzo hizo.
Kupitia Tuzo hizo Tanzania itazidi kujitangaza katika sekta ya utalii kwa jumla pamoja na kukuza Muziki wa Bongo Fleva nje ya Tanzania.