Kwa Nini LYNN Asilindwe?

BAADA ya minong’ono ya hapa na pale kumhusu msanii wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lynn’ kutinga na mabaunsa wanne kwenye sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Dunken House maeneo ya Mikocheni, Dar, mwenyewe amesema alifanya hivyo kutokana na uzuri alionao.

 

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa, Lynn alisema watu wanaona kitu gani cha ajabu yeye kulindwa na mabaunsa kwani ni jambo la kawaida ukizingatia yeye ni msichana mrembo anayetakiwa kulindwa siku zote.

 

“Watu wanashangaa kwa nini ninalindwa na mabaunsa? Kwani hawajui mimi ni msichana mrembo ninayestahili kulindwa? Mimi nitalindwa wakati wowote,” alisema Lynn aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Mondi’.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment