KWA NINI TANASHA HAKUBALIKI KWA MONDI?

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Na Mpenzi wake Tanasha Donna.

JARIBIO halipo mbali. Halichukui muda mrefu sana kutoa majibu. Cha kufanya, chukua picha kali ya mrembo Tanasha Donna. Hakikisha ina mvuto wa kutosha. Usiandike neno lolote la kuonesha upo upande gani kisha weka picha hiyo kwenye ukurasa wa mtandao wowote wa kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram au WhatsApp.

 

Dakika kadhaa baadaye, fungua sehemu ya “comments” (maoni), utakutana na majibu juu ya kwa nini mashabiki lukuki wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hawamkubali mchumba’ke wa sasa, Tanasha Donna Oketch.

 

Tanasha ni mtangazaji mrembo kutoka nchi jirani ya Kenya. Ana takriban miezi mitatu tangu aingie kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond ambaye ni mwanamuziki wa kimataifa anayepeperusha vyema bendera ya Bongo Fleva.

 

Katikati ya mapenzi motomoto baina ya wawili hao huku jamaa akimmwagia sifa kedekede, baadhi ya mashabiki wa Diamond au Mondi wameendelea kuwa vichwa ngumu. Hawakubali kusikia Diamond anamuoa Tanasha. Ndiyo maana wakati Diamond anatangaza kuahirisha zoezi la kufunga ndoa na Tanasha lililopangwa kufanya Februari 14 (Valentine’s Day), mwaka huu, kuna watu walichekelea meno thelathini na mbili yote nje.

Walio upande wa Tanasha wameendelea kubaki wachache. Mbali na Mondi ambaye hilo ndilo chagua lake ambalo upende usipende anasikiliza matakwa ya moyo wake, wengine ni mama yake, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na dada’ke, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.

 

Dada yake mwingine, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ hana habari na Tanasha, yeye bado anamuota Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni ‘eksi’ wa Mondi aliyezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan. Watu kama kaka’ke, Rommy Jones huwa wanafuata tu anavyotaka Mondi.

Wengine ni waja ambao kazi yao ni kudandia ishu za watu. Hawa hata kama Mondi angesema anamuoa msichana asiyejulikana huko Tandale-Magharibi wangeshadadia na kumsifia. Mfano wao niJuma Lokole. Lakini kwa nini baadhi ya watu hawamkubali Tanasha? Uchunguzi wa Gazeti la Risasi Mchanganyiko una majibu;

 

VIATU VYA ZARI HAVIVALIKI

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, bado wasifu wa Zari ni maji marefu kwa Tanasha. Wapo wanaokiri kuwa viatu vya Zari havivaliki kirahisi. Ama vinambana au kumpwaya Tanasha. Wengi wanasema kuwa Zari ni mama bora kwani ni mama wa watoto watano, lakini amekuwa mfano bora kimalezi, kipimo ambacho kwa Tanasha hakipo.

MVUTO WA NJE

Achana na mambo ya kuwa mama bora, lakini vipimo vya nje vinaonesha kwamba wapo ‘ma-ex’ wa Diamond wanamzidi Tanasha ambaye hafi kii kiwango chao cha mvuto wa kimaumbile. Pamoja na kuwa na umri mdogo wa miaka 23, lakini hafui dafu kwa Zari anayegonga umri wa miaka 40 au Wema mwenye 30. Mfano unaotumika ni ‘kifua’ chake kulegea mapema kabla hata ya kunyonyesha.

 

N YOTA

Ipo ishu inayozungumzwa zaidi ya nyota. Wakati Mondi akiwa na kina Wema Isaac Sepetu au Zari, nyota yake iling’aa mno. Wapo wengi ambao wanaamini kwamba nyota ya Tanasha imepoa ukilinganisha na Wema, Zari na hata Hamisa Mobeto.

NGUVU YA MA-EX WENGINE

Ukweli mwingine mchungu ni kwamba Tanasha anazidiwa na wingi wa wafuasi wa ma-ex wa Mondi. Kwa haraka haraka ukitazama kwenye kurasa zao za Instagram, Tanasha ana wafuasi kiduchu ambao ni laki 3.5 ukilinga  nisha na Zari mwenye wafuasi milioni 4.9, Wema milioni 4.5 na Mobeto milioni 3.3 hivyo nguvu ya umma ndiyo inayoongea!

Toa comment