Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kwa wasomaji wa Magazeti Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda yanayosambazwa nchi nzima, na Global Publishers.
JINSI YA KUSHIRIKI
Msomaji atatakiwa kununua nakala moja au zaidi ya magazeti tajwa na kukata kuponi moja iliyomo ndani ya magazeti hayo. Atatakiwa kujaza jina lake kamili na anwani yake na kisha kuituma kwa njia ya posta au kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers au kwa mawakala wake waliyopo sehemu mbalimbali nchini. Kwa wale wa mikoani, nao wanaweza kutuma moja kwa moja kwa mawakala wetu au kutuma kwetu kwa njia ya posta. Kutakuwa na vituo vya kukusanyia kuponi katika kila kata na mitaa mbalimbali nchini Tanzania.
MASHARTI
Wasomaji wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 wanaruhusiwa kushiriki, lakini wafanyakazi wa Global Publishers, waandishi wake na ndugu zao hawaruhusiwi kushiriki. Msomaji anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya Nyumba na zawadi nyingine. Kuponi zote zitaingia katika droo ndogo na kubwa.