#GlobalUpdates: Kwa Wale Wanaopenda Kujiachia, Instagram Kuanza Kuficha Picha Na Videos Za Utupu! – (Pichaz)

Instagram wanazidi kuboresha matumizi ya App yao ikiwa ni sehemu ya ahadi waliyoitoa September mwaka jana kuifanya App hiyo ‘sehemu salama kwa matumizi ya kila mtu‘, na kama ilikuwa haijakufikia bado ipokee update nyingine kutoka kwao.

Wakiendelea kutimiza ahadi waliyoitoa September mwaka 2016 kuifanya Instagram ‘sehemu salama kwa watu wote’ App hiyo inayomilikiwa na Facebook imetangaza mabadiliko kadhaa yatakayo hakikisha Instagram inakuwa sehemu salama kwa watumiaji wake wote wakubwa na wadogo.

Instagram imetangaza kuanza ‘kuficha picha na videos za utupu’ zinazopanda na kuonekana kwenye App hiyo. Licha ya hayo mtandao huo umetangaza kuanzisha page itakayomuwezesha mtu kujifunza namna ya kuepukana na jinsi ya kujilinda na picha pamoja na video za namna hiyo.

 

Kupita blog yao, Instagram walitoa taarifa hiyo inayosema:

“ Soon you may notice a screen over sensitive photos and videos when you scroll through your feed or visit a profile. While these posts don’t violate our guidelines, someone in the community has reported them and our review team has confirmed they are sensitive. This change means you are less likely to have surprising or unwanted experiences in the app. If you’d like to see a post that is covered with a screen, simply tap to reveal the photo or video. 

Japo taarifa hii haikatazi au kuzuia moja kwa moja watu kupost picha ama videos za utupu, kupitia post waliyoiweka kwenye page yao ya Instagram, Instagram wamesema wameamua kufanya mabadiliko hayo kwani mtu anaweza akaripoti kukwazika na video ama picha za namna hiyo na pale team ya uchunguzi ikijiridhisha kuwa picha ama video hiyo inakwaza basi hatua zitachukuliwa. 

Kuisoma yote kwa urefu gusa hii link ya blue.

TUBONGE: Wewe unaonaje, hapa Instagram wanajenga ama wanabomoa? Na kipi bora, kuzuia moja kwa moja picha na videos za utupu, ama kuzificha inatosha?

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.


Toa comment