The House of Favourite Newspapers

Kwa Yanga hii, Mtapigwa Nyingi Sana!

0

YANGA juzi ilitangaza kamati mpya ya mashindano ambayo inaongozwa na matajiri, watoto wa mjini waliowahi kuipa makombe saba Yanga kabla ya kujiweka kando.


Kamati hiyo iliyotangazwa na
Mwenyekiti wa timu hiyo, Dr Mshindo Msolla juzi, inaongozwa na mwenyekiti wake Rodgers Gumbo wajumbe ni Hamad Islam, Lucas Mashauri ambao wote ni watu wa kazi kweli.

 

Wengine ni Abdallah Bin Kleb, Davis Mosha, Seif Magari, Injinia Hersi Said, Pelegrinius Rutayunga na Arafat Haji.Bin Kleb na Seif Magari wanakumbukwa kwa umafia mkubwa walioufanya wa kuwapoka Simba kiungo mkabaji, Mbuyu Twite ambaye alitangazwa na aliyekuwa mwenyekiti wake Ismail Rage lakini baadaye akaja kuibukia Yanga msimu wa 2014/2015.


Pia walifanya umafia mwingine wa
kumuiba Kelvin Yondani waliyemchukua kutokea Simba katika msimu wa 2012.Katika kipindi hicho walikuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Mosha katika kuhakikisha wanafanya usajili wa nguvu wa kuchukua makombe huku mwenyekiti akiwa Yusuf Manji.

 


Achana na umafia huo, chini ya
wajumbe hao Yanga ilifanikiwa kuchukua makombe saba kwa kuanzia msimu wa 2012/ 2017. Katika kipindi hicho Yanga ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu mara nne kati msimu wa 2012/2013, 2014/2015, 2015/ 2016 na 2016/ 2017.

 

Ngao ya Jamii wamechukua mara mbili mfululizo msimu wa 2013/ 2014 na 2014/ 2015 kwa mara zote wakiifunga Azam FC. Katika uongozi wao huo, kamati hiyo ilifanikiwa kubeba Kombe la Kagame, mara moja mwaka 2012 ambalo hadi leo hii hawajalichukua tena.

 

Hii ni alama kwa timu zote ikiwemo Simba kuwa sasa moto utawaka na kama kuna timu itaenda kichwakichwa itapigwa nyingi sana kutokana na jinsi watu hao wanavyofahamu fitina za soka la Bongo.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply