The House of Favourite Newspapers

Kwenye Warsha ya Takukuru, DC Kinondoni Ataja Idadi ya Watoto Wanaobakwa kwa Siku, Idadi Inatisha!

Kaimu Mkuu wa Takukuru Manispaa ya Kinondoni, Christian Nyakizee akizungumza kwenye mkutano na wahabari ofisini kwake (hawapo pichani) leo.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Manispaa ya Kinondoni leo imetoa taarifa miezi mitatu ya harakati zake za kupambana na vitendo vya rushwa ambapo pamoja na mambo mengine imefanya warsha na maofisa wa polisi na maofisa wa ustawi wa jamii ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule ambaye katika risala yake kwenye warsha hiyo alitaja idadi ya watoto wanaobakwa na kulawitiwa kwa siku pamoja uhalifu mwingine wa masuala ya rushwa na kuahidi kukomesha uhalifu huo kwa kushirikiana vyema na Takukuru.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar Kaimu Mkuu wa Takukuru Manispaa ya Kinondoni, Christian Nyakizee amesema idadi hiyo iliyotajwa na mkuu huyo wa wilaya ya idadi ya watoto wanaobakwa na kulawitiwa kwa siku inatisha jambo linaloonesha kuporomoka kwa maadili na kuahidi kukomesha vitendo hivyo.

Nyakizee amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari juu ya warsha walizofanya na maofisa wa polisi dawati la jinsia pamoja na maofisa wa ustawi wa jamii juu ya kukomesha matendo hayo.

Akielezea warsha hizo za kimafunzo Nyakizee amesema Agosti 30 mwaka huu walitoa mafunzo ya kuzuia uhalifu huo na maofisa wa ustawi wa jamii 25 kutoka Kata za Manispaa ya Kinondoni kwenye Ukumbi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni.

Warsha ya maofisa ustawi wa jamii ilifuatiwa ya maofisa wa polisi iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Septemba 26 mwaka huu.

Nyakizee ameendelea kusema mafunzo hayo yalihudhuriwa na askari polisi 37 kutoka katika madawati na jinsia 14 kutoka Manispaa ya Kinondoni ikiwemo, Kituo cha Oysterbay, Kijitonyama, Chuo Kikuu UDSM, Magomeni, Urafiki, Mburahati, Gogoni, Magufuli Bus Terminal, Mavurunza, Kawe, Mabwepande, Goba na Madale.

Katika Warsha hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule ambaye alisema takwimu zinaonesha katika wilaya hiyo kipindi cha Julai mwaka huu watoto 36 walibakwa na kulawitiwa na Agosti mwaka watoto 29 walibakwa na kulawitiwa. Alisema Nyakizee.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

SHOMBO za AHMED ALLY – “YANGA WAMEFUNGASHWA -KULE SIYO KUFUNGWA -WAMELAMBISHWA ASALI MBICHI”