Kylie Jenner avalishwa pete ya uchumba

KYLIE JENNER (3)Licha ya kugombana mara kwa mara na kufikia hatua ya kufunguliana mashtaka, Kylie Jenner akidai mpenzi wake Micheal Ray Stevenson ‘Tyga’ amemuibia pesa, sasa wapenzi hao wamefungua ukurasa mpya kwa kuingia kwenye hatua ya uchumba.

KYLIE JENNER (1)Tyga alifikia hatua ya kumvisha pete baby wake huyo pete ya uchumba baada ya kuona hakuna mwingine zaidi yake na inadaiwa sasa hivi penzi limenoga ile mbaya.

KYLIE JENNER (2)Kwenye tukio la kuvalishana pete, Tyga alifanya kama sapraizi kwani hakumpa taarifa na chanzo kinadai kuwa mama Kris Jenner ambaye ni mama wa Kylie alishuhudia lakini hakuamini, aliona kama maigizo tu.

KYLIE JENNER (4)Hata hivyo, inadaiwa Tyga alikuwa siriasi na kikubwa alikuwa akitaka penzi lao liwe rasmi, ikibidi wasichukue muda mrefu kabla ya kuoana.

KYLIE JENNER (5)Mara ya mwisho Kylie na Tyga walikuwa kwenye ugomvi mkali ambapo Kylie alidai kuwa Tyga anamsaliti na kuamua kuachana naye, baadaye wakarudiana.

Toa comment