Watu 23 Wafariki Shambulio la Moto Katika Studio Japan

WATU zaidi ya 23 wamefariki leo (Alhamisi) katika studio ya kurekodi matangazo na kuchapisha vitabu na majarida mbalimbali katika vyombo vya habari mjini Kyoto, Japan, maofisa wa zimamoto wamesema. 

Idara ya zimamoto ya Kyoto imethibitisha kwamba watu 13 wamefariki na zaidi ya kumi walikutwa hawajitambui ndani ya jengo hilo linalomilikiwa na kampuni ya  Kyoto Animation Co.

Nchini Japan, maofisa wa serikali hutumia neno “kutojitambua” kuelezea vifo vya watu ambao chanzo cha vifo vyao vinakuwa havijathibitishwa rasmi.

Polisi wa Kyoto wamesema mtu mmoja alimwaga kile kilichoonekana kuwa petroli kuzunguka studio hiyo na kuwasha moto.  Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 41 amekamatwa na polisi.
Idara hiyo imesema watu zaidi ya 38 wamejeruhiwa na kumi wanasemekana kuwa katika hali mbaya kutokana na moto huo ulioanza mapema leo ambapo magari 48 ya zimamoto yalikuwa yamepelekwa kuuzima moto huo.

Loading...

Toa comment