The House of Favourite Newspapers

Lady Jaydee Kaolewa na Rastaman?

lady-jaydee-1Staa wa Bongo Fleva, Lady Jaydee ‘Anaconda’  akiwa katika matembezi na Rastaman.

lady-jaydee-2

Wakiwa katika mazungumzo matamatam katika Hoteli ya Serena visiwani Zanzibar.

.lady-jaydee-3

Akimshangaa Rastaman.

PICHA za staa wa Bongo Fleva, mwanadada Lady Jaydee ‘Jide”  zimenaswa akijiachia na mwanamme mmoja mwenye nywele za rasta ‘Rastaman’ sehemu mbalimbali.

Hizo ni picha za kwanza kuvuja zikimuonesha Jide akiwa beneti na mwaname kiasi cha watu kuhisi pengine ni mpenzi wake mpya baada ya kutengana na aliyekuwa mumewe, mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM,  Gardiner G Habash miezi kadhaa iliyopita.

Picha hizo zimeibua sintofahamu kwa mashabiki wa Jide wakijaribu kudadisi kama kweli Rastaman huyo  ndiye shemeji yao.

Mtandao huu ulinyanyua waya na kumpigia meneja wa msanii huyo, Seven ili aweke bayana kuhusu ukweli wa picha hizo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Comments are closed.