The House of Favourite Newspapers

Lalji Foundation Yatoa Msaada wa Viungo Bandia kwa Watoto 11 CCBRT

0

 

TAASISI isiyo ya kiserikali ya LALJI FOUNDATION imetoa msaada wa viungo bandia kwa watoto 11 waliopo katika hospitali CCBRT Dar es es salaam ikiwa ni katika kurudisha furaha ya watoto hao na vilevile kuongeza ushiriki wao kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa LALJI FOUNDATION ndugu Imtiaz Lalji amebainisha kuwa lengo ni kugusa watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii ambapo pia amewataka wadau na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi hizo.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya CCBRT Brenda Msangi ameishukuru taasisi hiyo kwa kutoa msaada huo na kubainisha kuwa bado mahitaji ni makubwa ambapo mpaka sasa kuna zaidi ya wagonjwa 800 wanaohitaji kupatiwa viungo saidizi.

Leave A Reply